NYOTA WA GHANA, CHRISTIAN ATSU AFARIKI DUNIA UTURUKI


MWILI wa mwanasoka wa Ghana Christian Atsu umepatikana chini ya jengo alilokuwa akiishi kusini mwa Uturuki baada ya tetemeko kubwa la ardhi wiki iliyopita.
Wakala wa winga huyo wa zamani wa Chelsea amenukuliwa na Reuters akielezea kifo cha nyota huyo wa Ghana ambaye alikuwa anachezea Hatayspor ya Ligi Kuu ya Uturuki.
"Mwili wa Atsu ulipatikana chini ya vifusi," Murat Uzunmehmet aliwaambia waandishi wa habari huko Hatay, ambapo mwili wa mwanasoka huyo ulipatikana.
"Kwa sasa, vitu zaidi bado vinatolewa. Simu yake pia ilipatikana." 
Atsu alikuwa amepanga kusafiri Kusini mwa Uturuki saa chache kabla ya tetemeko hilo kutokea, lakini alisema Ijumaa Mghana huyo aliamua kusalia na klabu hiyo baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi ya Februari 5 ya ligi ya Uturuki (Super Lig).
Atsu aliwahi kuichezea Newcastle United pia. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.
WASIFU WA MAREHEMU CHRISTIAN ATSU
Jina Kamili Christian Atsu Twasam[1]
Tarehe ya Kuzaliwa 10 January 1992
Mahali Alipozaliwa Ada Foah, Ghana
Tarehe ya Kifo chake c. 6 February 2023(aged 31)
Mahali Alipofia  Antakya, Turkey
Ukubwa wa mwili 1.65 m (5 ft 5 in)[2]
Nafasi aliyekuwa anacheza Winga
Timu za Vijana
Feyenoord Fetteh
Cheetah
2009–2011 Porto
Timu za Wakubwa
Mwaka Timu Mechi (Mabao)
2011–2013 Porto 17 (1)
2011–2012 → Rio Ave (loan) 27 (6)
2013–2017 Chelsea 0 (0)
2013–2014 → Vitesse (loan) 28 (5)
2014–2015 → Everton (loan) 5 (0)
2015–2016 → Bournemouth (loan) 0 (0)
2016 → Málaga (loan) 12 (2)
2016–2017 → Newcastle United (loan) 32 (5)
2017–2021 Newcastle United 75 (3)
2021–2022 Al-Raed 8 (0)
2022–2023 Hatayspor 3 (1)
Total 207 (23)
Timu ya Taifa
2012–2019 Ghana 65 (9)


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA