SIMBA WAKAMILISHA KAMBI YA SIKU 17 MOROCCO

 MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamekamilisha kambi yao ya siku 17 nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya na wataondoka kesho kurejea Dar es Salaam.
Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba awamu ya pili ya mazoezi ya kujiandaa msimu itaanza baada ya kurejea kwa wachezaji wa klabu hiyo waliopo kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mapema mwezi ujao.
Simba iliyowasili Morocco Agosti 11, katika kambi hiyo ya wiki mbili na ushei Jijini Rabat ilipata pia na mechi mbili za kirafiki na zote ilitoa sare 1-1 na Khourigba na 2-2 na Rabat.


Dhidi ya Khourigba, kiungo Papa Ousmane Sakho alianza kuifungia Simba dakika ya 37, kabla ya Mseegal mwenzake, mshambuliaji Adama Diom kuwasawazishia wenyeji dakika ya 61.
Na dhidi ya FAR Rabat, mabao ya Simba yalifungwa na viungo Hassan Dilunga dakika ya 54 na Sakho dakika ya 81 baada ya FAR Rabat kutangulia kwa mabao ya Chabani dakika ya 14 na Abba dakika ya 26.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA