KABLA YA KUWAVAA KMC, BIASHARA UNITED HALI NI TETE, KUWAKOSA WACHEZAJI TISA
KOCHA Mkuu wa timu ya Biashara United, Amri Said amesema kwa sasa timu yake ipo kwenye hali mbaya kiuchumi hali inayofanya wajiendeshe kwa kuungaunga.
Said amesema kukosekana kwa mdhamini mkuu kunaathiri ubora wa ligi kwani wachezaji wamekuwa katika mazingira magumu huku kikosi chake cha kwanza kikiwa na wachezaji watatu pekee ambao ni wazima.
Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema atawatumia wachezaji wa kikosi cha pili kutokana na wachezaji 9 wa kikosi cha kwanza kusumbuliwa na malaria na wengine kusumbuliwa na majeraha.
"Tunapitia kwenye kipindi kigumu kwa sasa kwani ligi ni ngumu na kila timu inatafuta matokeo, kikosi changu kipo sawa ila nitawakosa wachezaji wangu muhimu 9 kwenye mchezo wangu dhidi ya KMC.
"Nimewavuta vijana wa timu b kwa ajili ya kutafuta matokeo, uchumi kwetu ni mgumu na mambo ni mengi kwetu, hivyo wadau watupe sapoti katika hili maana hakuna namna tunajikongoja kwa sasa," amesema Said.
Biashara United itamenyana na KMC uwanja wa Uhuru Jumamosi Marchi 2, huku wakiwa nafasi ya 19 baada ya kucheza michezo 26 na wana pointi 23 huku wapinzani wao KMC wakiwa nafasi ya nne na pointi 40 baada ya kucheza michezo 27.
Comments
Post a Comment