MISRI NA SENEGAL ZAKAMILISHA NUSU FAINALI AFCON


TIMU ya taifa ya Senegal imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Equatorial Guinea usiku huu Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Cameroon.
Mabao ya Simba wa Teranga yamefungwa na Famara Diedhiou dakika ya 28, akimalizia pasi ya Sadio Mane, Cheikhou Kouyate dakika ya 68 na Ismaila Sarr dakika ya 79, wakati la Equatorial Guinea limefungwa na Jannick Buyla dakika ya 57.
Awali ya hapo, Misri ilitangulia Nusu Fainali kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Morocco hapo hapo Ahmadou Ahidjo katika mchezo uliodumu kwa dakika 120.
Sofiane Boufal alianza kuifungia Morocco kwa penalti dakika ya sita na Mohamed Salah akaisawazishia Misri dakika ya 53, kabla ya nyota huyo wa Liverpool kumsetia Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan ‘Trezeguet’ kufunga la ushindi dakika ya 100.
Sasa Misri itakutana na wenyeji, Cameroon Alhamisi baada ya Senegal kumenyana na Burkina Faso katika Nusu Fainali ya kwanza Jumatano.



Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA