SOKA YA TANZANIA BADO NI RIDHAA, SI YA KULIPWA KAMA TUNAVYOAMINI

Na Ally Msigwa, IRINGA
Kwa Tanzania, Soka ni Ajira kama Ajira zingine  Huku Tukiamini Ni Sahihi, Tunaamini Soka ni Professionalism kwa Aspect ya Mikataba na Renumeration clauses ila Je,  misingi ya ajira inafuatwa kisheria?Je, Viongozi na wachezaji wako kiprofessional in a Grassroot Descipline Level and operation? 
Kosa kubwa kwetu kufanya Soka letu ni Professional football, Wakati hata level ya semi Professional bado.. Ni rahisi soka la Tanzania hapa lilipo kushuka na kuporomoka kuliko kupanda mbele..
Hatujatatua misingi , hatujaanda nguzo za kuwa pro hatujaandaa mentality na mindset kuelekea Pro
Tulichofanya, tumelipamba hili soka kwa nakshi nyingi zinazo attract professionalism na competitiveness katika ngazi ya mavuno zaidi.
Tanzania tumefanikiwa kuendesha soka kwa mikataba na kutoheshimu mikataba yenyewe kwa yale ambao pande mbili wamekubaliana. Najua tunafahamu kesi nyingi sana juu ya mikataba kwa baadhi ya Vilabu kutofuata taratibu pia hili linatokea kwa wachezaji pia, Na mbaya zaidi kuna tabia kwa baadhi ya vilabu kuwatumia wachezaji ambao awajasajiliwa kwenye ligi husika na kutumia jina la mtu mwingine kwa kufoji picha.
Hapa ndipo ambako tunatakiwa kujua mchezaji ameandaliwa kuishi kipro ndani ya uwanja na nje ya uwanja,Nikweli maisha ya wachezaji wetu yapo kipro? Ni kweli wachezaji wetu wameandaliwa hata kujua kuongea na media? Wachezaji wetu wanatambua haki zao kwenye matangazo aidha ya klabu au tangazo lake mwenyewe? Wachezaji wetu wanatambua vyakula na Vinywaji wanavyotakiwa kula? Wachezaji wetu wanatambua sehemu ambazo wanatakiwa kwenda au kutokwenda? Wanaishije na jamii? Wachezaji wetu wanaweza kutokea majumbani kwao bila ya kukaa kambini pamoja na kuwa na kiwango kizuri kinachokidhi huduma ya soka la Ushindani kwa msimu mzima?  Kuna mengi sana hapa, hivi hata kwa viongozi husika pia wanasifa, exposure , experience na qualifications za kuongoza, kuratibu na kufuata taratibu za Uendeshaji Soka  kipro nchi hii kwa Asilimia ngapi? Utatafuta Tathmini kuanzia Ngazi za chini kupanda , Huko sifiki leo..
Kuna mjadala unaendelea wa Mh waziri juu ya kupunguza idadi ya wachezaji kutoka 10-5, haya yote kwangu yanaongelewa ila mzizi mkuu ni hili jambo wachezaji wetu wangekuwa na misingi ya kipro sidhani kama mjadala huu ungekuwepo ingawa hii pia ni mada nyingine..
Asilimia kubwa ya wachezaji wa ligi kuu hawalipwi stahiki zao ukiachilia kipindi hiki hawako kazini kama ilivyo ndugu zangu wa kampuni za waarabu na wahindi waliolipwa siku 20 na kulipwa nusu mshahara bila any negotiation wala compliance sababu ya CORONA .. FANYA TATHMINI...!
Kama hata kwenye mikataba hatuko sahihi hio professionalism iko wapi? Soka ina professional level kimisingi na kimfumo, tunatazama vingi kuanzia makuzi ya mchezaji ,mapitio yake katika angle za kisoka kujiridhisha ni Pro sahihi ndani na nje ya Uwanja pamoja na Ufikiri ili wanapoingia katika soko la Ushindani wapate kuwa treated kipro.
Tanzania hatuna hio Professional.BADO! Sipingi mtu akiwaza Semi pro kwa kuoneana aibu , ila in reality tumetia soka letu Nakshi nyingi za kipro na hatujajiandaa kimisingi ya kuwa Professional Hasa bali ya kuonekana Professional ATLEAST!...
Professional ni kazi kubwa sana ku Attain ..Hapa kuna mambo mengi sana yanatakiwa yafanyike ili tuweze kufika level hiyo..
Kuandaa tu mchezaji professional unahitaji kwa uchache miaka 10 kupata Professional graduate kimsingi..Tunahitaji Mno Kuandaa misingi ya Kuwa Professional football league na kuandaa Players ambao ni Professional kimisingi na Ki mentality, na ku operate Ajira za Soka katika daraja sahihi la kiPro ili kuanza kupiga hatua .. Asilimia kubwa ya wachezaji wa kitanzania hawadumu kwenye soka la ushindani na Professional level sababu kubwa ya kutofua dafu Soka la nje ya nchi sio ufinyu wa Vipaji bali tunagundulika Hatuna misingi sahihi ya Professional Football, Tuna Ajira za Soka na nakshi za Kiprofessional katika malipo ya kimkataba kama Ajira zingine ila still zinakuwa AJIRA KAMA AJIRA ZINGINE, hatuziheshimu ki Professional..
Tukiendesha hili Soka seriously, na kuweka misingi stahiki na sahihi kwa mujibu wa mahitaji ya standards za taaluma ya Soka na maendeleo yake ,nina hakika tutafika mbali sana.
Tanzania tumejaaliwa vipaji vya Hali ya juu Ukitazama idadi ya Watanzania walio lowea Nchi za Nje na kufanya vyemakisoka utakubaliana na mimi ya kuwa tukipata mafunzo sahihi ya Football na tukawekeza seriously bila Siasa tutapata kina Samatta wengi sana,Na hapa serikali itapata faida kubwa kwa mapato na kuitangaza Tanzania nashauri wapatikane wataalamu kila mkoa na wilaya ikiwezekana.
Pia zipatikane Centres kila mkoa au kila kanda hili lifanywe na serikali na tuanze kuwekeza kwenye shule za msingi ambako ndio kwenye umri sahihi kabisa, Hapa ndio tunaanza kuwafundisha mpira na kuwaandaa kabisa kuja kuwa pro, Pili serikali itoe misimamo na Sheria iliyo sahihi kabisa katika suala zima la kimikataba na ufuatiliaji makini kabisa  kupitia BMT na vyama vingine ingawa hapa wahusika wakuu ni TFF pia wachezaji mishara yao ianze kukatwa na kuliingizia pato serikali,Wachezaji wakatiwe BIMA kubwa,Malipo mifuko ya jamii kama NSSF,Pia makato kwenye chama cha wafanyakazi Nk, ili baada ya kustaafu kucheza aweze kulipwa mafao yake pia, Hapa itaweza kumsaidia kama wakati wa kucheza akuweza kuwekeza ambacho atapata kinaweza kumsaidia kuendesha Maisha yake.Tukiamua na kujipa muda kuanzaa sasa na hakika baada ya miaka 10 Tanzania itakuwa mbali sana . Tuwawekee watoto wetu misingi iliyokuwa bora na ya kisasa zaidi ili nasisi tuwe kwenye mzunguko sahihi wa soka la dunia na hapa kujifunza na kuiga kwa walioendelea sio dhambi tuamue kwa pamoja ila nasisitiza mambo haya yanatakiwa kufanywa na wataalamu wa soka sio kuleta SIASA au Mkakati Zimamoto .
Asanteni sana nawatakia Ramadan Kareem na tukumbuke kujilinda na CORONA. 🙏🏻🇹🇿⚽
Safari tunayo Ndefu kama Tutaamua Tunaweza Piga Hatua...*`
(Ally Msigwa ni mchezaji wa zamani wa Yanga, mdau wa soka na kiongozi wa soka Iringa ambaye anapatikana kwa namba +255 717 787 357)


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA