KUNA TATIZO ZAIDI YA IDADI YA WACHEZAJI WA KIGENI LIGI KUU

Na Ibrah Mkemia, DAR ES SALAAM
WAKATI dunia ikipambana na ugonjwa hatari wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya covid_19 (corona) ambao umeonekana ni tishio, na kuua watu wengi katika baadhi ya nchi. Hali hii imesababisha shughuli nyingi sana kusimama. Ikiwemo soka na hata shughuli za kiuchumi. 
Baada ya janga hili kutokea, kumeibuka mijadala mingi kuhusu michezo. Hasa katika kandanda hapa naamanisha mpira wa miguu. Ipo mijadala kuusu umalizaji wa ligi katika nchi husika, kupanda na kushuka daraja. Lakini mjadala ambao umenifanya nishike kalamu nyeusi na niweze kuandika ni kuhusu mjadala amabo umetokea katika mjengo ambao wawakilishi wa majimbo (wabunge) hukutana na kujadili mambo yanayoihusu nchi yetu Tanzania.

Mshambuliaji Mzimbabwe wa Azam FC, Donald Ngoma akimiliki mpiraa mbele ya beki Mganda wa Lipuli FC, Joseph Owino katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Mjadala kuhusu wachezaji wa kigeni. Huu ni hoja ambayo imetolewa na waziri mwenye dhamana ya michezo. "Kupunguza wachezaji wa kigeni kutoka wachezaji kumi (10) ambao wapo kwa sasa hadi kufikia wachezaji watano (5). Hii hoja imeamsha hisia za wapenda mpira wa miguu nchini,  Na kila mmoja kuja na hoja yake.
Wengi wameongea, wengine wakisema wapunguzwe kama asemavyo waziri. Lakini wengine wameenda mbali kabisa wakisema ikiwezekana waongezwe na kusiwe na kikomo cha wachezaji wa kigeni. 
Jicho la mdau " Nikianzia katika vyombo vya habari (media) vimejitahidi kuweka vipindi vingi vya kuhusiana na michezo hasa mpira wa miguu hili halina ubishi. Pia vimejitahidi kuweka wachambuzi wengi ambao wamekuwa na weledi wa kulizungumzia soka kwa undani zaidi, kama sio kuchambua tuko wapi, tunafanya nini, tunapita wapi,  na tumekosea wapi? Hayo ni maswala ambayo vyombo vya habari vimejitahidi kwa upana wake kwa ajili ya wapenda soka.
Lakini tatizo kubwa kwa watanzania tumekuwa watu wa kuchukilia poa vitu vinavyosemwa na hao wachambuzi (kupuzia) bila kujua mtu huyo mchambuzi au mtu wa michezo ana utaalamu gani kwenye nyanja ya kimichezo hasa mpira wa migu.
Tuje kwenye ufahamu wa wapenda soka hilo sasa. Wengi wetu tunalichukulia kandanda tunavyoliona uwanjani. Na sio kiufundi zaidi na hili ndo linakuwa tatizo. Hapa sasa ndo tunatakiwa kuwaachia wachambuzi na wajuzi wanyanja mbalimbali za kiufundi kwenye kandanda".
Tanzania kumekuwa na utamaduni sijui ndo tuseme ni mazoea ya baadhi ya watu kutotazama mbali hasa katika upande wa soka. Wengi wetu tumeweka maslai ya vilabu vyetu kwa maana ya ushabiki baada ya kuweka utaifa mbele. Inabidi tuache kwa sababu hii dhambi itaendelea kututafuna kila tunapopiga hatua moja mbele.
Ni vyema kwa sasa kila mtu akashika jukumu lake Kiungozi. Kwa kuangalia mambo yafuatayo:- Ufundi, Miundombinu, Utawala, Mawasiliano nk. Sisemi kuwa waziri kuzungumzia suala la kupunguza wachezaji wa kigeni sio jukumu lake. Lakini je swala hilo limepelekwa kwa wataalamu wa ufundi wa Tff au balaza la michezo la taifa (BMT).
Kama tuanaka kuendelea na kuboresha soka letu la Tanzania ili tuweze kupambana na nchi nyingine barani afrika na hata ulaya. Ni vyema kuaminiana. Maisha ya taifa la soka yanahitaji wanasoka. 
Hatujafikia hatua ya kuzidiwa mpira na wageni wachache kwenye mpira wetu. Namaanisha wachezaji wa kigeni. La msingi ni kuboresha sehemu mbalimbali za kisoka kwa maana ya viwanja, makocha, na vifaa vinginevyo vinavyohusiana na kandanda.
Siamini kama tatizo la nchi na vilabu vyetu kufanya vibaya kimataifa ni wachezaji wa kigeni kujaa katika timu zetu. Shida ni ufinyu wa viwanja ambavyo vingeweza kuzalisha wachezaji wengi sana. Ikumbukwe Tanzania miaka ya 70' ilikuwa na watu wapatao milioni 35'. 
Tujiulize tokea hapo tumeongeza viwanja au tumpunguza sehem za wazi za watoto kucheza kandada. Jibu ni tumeongeza watoto tumepunguza viwanja vya kuzalisha wachezaji hili pia nalo ni bonge la tatizo.
Wataalamu wa wizara hawakuona hilo au wamefumba macho. Taifa halikuanza jana haya ndo matatizo ambayo yanatufanya tushindwe sio wachezaji wa kigeni. Sio naishambulia wizara bali najadili tulicholetewa wanasoka kuhusu wachezaji wa kigeni. BABA UKIONDOA KOFIA UWE NA KILEMBA.
Huu mzigo mzito na sio wa kumpa mnyamwezi wala haupimwi kwa macho. Tutaumia bila kujipanga. Na tusipo angalia utatuletea shida,   Huu mzigo begani haukai na kichwani ni tabu.
Tunaweza kuepuka kuvuruga taswira ya wanamichezo endapo tutatengeneza viwanja,  kama ilivyokuwa zamani watoto wengi wakacheza kuandaa walimu kwa ngazi ya vijana ili kuweza kukuza na kuanzisha soka la vijana. Pia katika eneo la waamuzi bora ili kupata haki viwanjani. Rushwa itazamwe timu zishindane kwa haki. Tunao wachezaji wanaojitambua.
Tunaweza bila kuondoa wageni. "BABA UKIONDOA KOFIA BASI UWE NA KILEMBA"

(Imeandikwa na Ibrah Mkemia @kalomoibrahim@gmail.com 0715147449)


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA