MAN CITY YAICHAPA PSG 2-1 ETIHAD
WENYEJI, Manchester City wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad.
Kylian Mbappe alianza kuifungia Paris Saint-Germain dakika ya 50, kabla ya Man City kuzinduka kwa mabao ya Raheem Sterling dakika ya 63 na Gabriel Jesus dakika ya 76 na kwa matokeo hayo zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora.
Manchester City inaongoza Kundi kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na PSG nane, RB Leipzig nne sawa na Club Brugge.
Comments
Post a Comment