MESSI AWEKA REKODI BALLON D’OR YA SABA


MUARGENTINA Lionel Messi ameweka historia baada ya kushinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya saba usiku wa Jumatatu ukumbi wa Theatre Du Chatelet  Jijini Paris, Ufaransa.
Messi amebeba tena tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 38 akiwa na Barcelona msimu uliopita kabla ya kuhamia Paris St Germain kama mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba.
Muargentina huyo amemshinda mshambuliaji wa kimataifa wa Poland na klabu ya Bayern Munich, Roberto Lewandowski na nyota wa Chelsea, Jorginho alioingia nao fainali.
Mpinzani wake wa muda mrefu kwenye kinyang’nyiro hicho, Mreno Cristiano Ronaldo ameshika nafasi ya sita na hakuhudhuria tafrija hiyo.
Messi pia anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya Ballon d’Or katika miongo mitatu tofauti.
Katika tuzo hiyo ambayo hutokana na kura za waandishi wa habari za soka 180 duniani kote, mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ameshika nafasi ya nne, Mfaransa mwenzake, kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante wa tano mbele ya Ronaldo.
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe kashika nafasi ya tisa na kipa wa zamani wa Juventus, Gianluigi Donnarumma amekamilisha 10 Bora.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA