TANZANIA YAMALIZA YA PILI COSAFA


TANZANIA jana imemaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya Soka la Ufukweni baada ya kufungwa 3-1 na Msumbiji katika Fainali ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban.
Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Msumbiji kwa Tanzania, kwani mechi ya Kundi B walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4.
Mechi nyingine Tanzania iliyo chini ya kocha Boniphace Pawasa ilishinda 3-1 dhidi ya Comoro Kundi A kabla ya kuifunga Angola 5-2 kwenye Nusu Fainali.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NI YANGA BINGWA KOMBE LA MUUNGANO 2025