Posts

Showing posts from April, 2021

TANZANIA PRISONS 0-1 YANGA SC (KOMBE LA TFF)

Image
 

YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 SUMBAWANGA BAO LA YACOUBA SOGNE

Image
 VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mburkinabe Yacouba Sogne dakika ya 54 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza. Yanga inaungana na Rhino Rangers ya Tabora, Biashara United ya Mara, Mwadui FC ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam pia kuwa timu zilizotinga Nane Bora hadi sasa. Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Dodoma Jiji FC na KMC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Simba SC na Kagera Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati keshokutwa JKT Tanzania watamenyana na Namungo FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kukamilisha Hatua ya 16 Bora.

SIMBA SC KUMENYANA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA MEI 15

Image
 TIMU ya Simba SC ya Tanzania itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya droo iliyopangwa leo Jijini Cairo nchini Misri. Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri nao watamenyana na wapinzani kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.  Mshambuliaji Mtanzania, Simon Happygod Msuva yeye timu yake, Wydad Casablanca itamenyana na MC Alger ya Algeria. CR Belouizdad ya Algeria pia yenyewe itamenyana na vigogo wengine wa Afrika, Esperance ya Tunisia. Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 14 na 15 na marudiano ni Mei 21 na 22, Simba SC wakianzia nyumbani Dar es Salaam. ROBO FAINALI Al Ahly vs Mamelodi Sundowns.  MC Alger vs Wydad Casablanca.  CR Belouizdad vs Esperance.  Kaizer Chiefs vs Simba SC.  NUSU FAINALI   MC Alger / Wydad Casablanca VS  Kaizer Chiefs / Simba SC.  CR Belouizdad / Esperance VS Al Ahly / Mamelod Sundowns.

MWADUI FC NAYO YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA COASTAL UNION 2-0 LEO SHINYANGA

Image
 TIMU ya Mwadui FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga. Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Roshwa Rashid dakika ya 14 na Wallace Kiango dakika ya 24. Mwadui FC inakamilisha orodha ya timu tatu tupu za mikoa inayopakana kufuzu Robo Fainali hadi sasa, nyingine ni Biashara United ya Mara na Rhino Rangers ya Tabora. Mchezo kati ta wenyeji, Tanzania Prisons na Yanga SC unafuatia hivi sasa Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

BEKI MKONGWE WA KULIA NCHINI, SHOMARI KAPOMBE ASAINI MKATABA MPYA WA KUENDELEA NA KAZI SIMBA SC

Image
BEKI mkongwe wa kulia nchini, Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simba SC.

MAN UNITED YATOKA NYUMA 2-0 NA KUICHAOA ROMA 6-2 OLD TRAFFORD

Image
 TIMU ya Manchester United imetoka nyuma kwa 2-0 na kushinda 6-2 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya UEFA Europa League Uwanja wa Old Trafford. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Bruno Fernandes mawili dakika ya tisa na lingine 71 kwa penalti, Edinson Cavani mawili pia dakika ya 48 na 64, Paul Pogba dakika ya 75 na Mason  Greenwood dakika ya 86, wakati ya Roma yamefungwa na Pellegrini Pellegrini 15 na Edin Dzeko dakika ya 33. Mechi nyingine ya Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA Europa League Villarreal imeshinda 2-1 dhidi ya Arsenal Uwanja wa Cerámica, huko Villarreal na timu hizo zitarudiana kesho.

BARCELONA YACHAPWA 2-1 NA GRANADA PALE PALE CAMP NOU

Image
 WENYEJI, Barcelona wamechapwa 2-1 na Granada katika mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Camp Nou. Mabao ya Granada yamefungwa na Darwin Machís dakika ya 63 na Jorge Molina dakika ya 79, wakati la Barcelona limefungwa na Nahodha wake, Lionel Messi dakika ya 23. Baada ya kipigo hicho Barcelona inabaki na pointi zake 71 katika nafasi ya tatu, nyuma ya Real Madrid yenye pointi 71 pia baada ya wote kucheza mechi 33, wakati Granada inafikisha pointi 45 za mechi 33 pia katika nafasi ya nane.

AZAM FC NA BIASHARA UNITED ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUZITOA POLISI TANZANIA NA RUVU SHOOTING LEO

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC katika mchezo huo wa michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) yote yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika za 25 na 65, wakati la Polisi limefungwa na Marcel Boniventura Kaheza dakika ya 76 kwa penalti. Mechi nyingine ya 16 Bora ya ASFC leo wenyeji, Biashara United wameitoa Ruvu Shooting kwa penalti 4-1 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Azam na Biashara zinaungana na Rhino Rangers ya Tabora kutinga Nane Bora ambayo jana iliitoa Arusha FC kwa kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

NAMUNGO FC YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KUNDI D KUCHAPWA 1-0 NA PYRAMIDS FC CAIRO

Image
 TIMU ya Namungo FC imekamilisha mechi zake za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuchapwa 1-0 na wenyeji, Pyramids FC usiku wa Jumatano Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo, Cairo. Bao pekee la Pyramids limefungwa na kiungo Mmisri, Ibrahim Adel dakika ya 65. Kwa matokeo hayo Pyramids inafikisha pointi 12 na kumaliza nafasi ya pili, nyuma ya Raja Casablanca yenye pointi 15 ambayo itakamilisha mechi zake kwa kumenyana na Nkana FC yenye pointi sita Jijini Casablanca nchini Morocco.

MAN CITY YAICHAPA PSG 2-1 PALE PALE PARIS

Image
TIMU ya Manchester City imetoka nyuma na kuwachapa wenyeji Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja Parc des Princes Jijini Paris nchini Ufaransa. PSG walitangulia kwa bao la Marquinhos dakika ya 15, kabla ya Kelvin De Bruyne kuisawazishia Man City dakika ya 64 na Riyad Mahrez kufunga la ushindi dakika ya 71. Man City watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo Uwanja wa Etihad. Ikumbukwe jana Real Madrid jana ililazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea Jijini Madrid nazo zitarudiana wiki ijayo London na washindi wa jumla wa mechi zote watakutana kwenye fainali Mei 29.

MANAHODHA WOTE WA SIMBA SC, JOHN BOCCO NA MOHAMMED HUSSEIN 'TSHABALALA' WASAINI MIKATABA MIPYA

Image
MANAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco na Mohammed Hussein 'Tshabalala' wote wamesaini mikataba mipya ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Nahodha Mkuu wa Simba SC, John Raphael Bocco amesaini mkataba mpya  Nahodha Msaidizi wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesaini mkataba mpya

MBEYA CITY YAFANYA BALAA ZITO LIGI KUU, YAITANDIKA JKT TANZANIA 6-1 SOKOINE

Image
 TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa 6-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 19, David Mwasa dakika ya 45 na ushei, Richardson Ng'ondya dakika ya 49, Juma Luizio dakika ya 68 na 88 na Pastory Athanas dakika ya 90 na ushei baada ya Danny Lyanga kuifungia JKT dakika ya nane. Kwa ushindi huo mnono, Mbeya City inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 28 na kusogea nafasi ya 13, wakati JKT inabaki na pointi zake 27 za mechi 27 sasa katika nafasi ya 17.

SIMBA SC 3-1 DODOMA JIJI FC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA CHELSEA NYUMBANI

Image
WENYEJI, Real Madrid wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid nchini Hispania. Kiungo Mmarekani Christian Pulisic alianza kuifungia Chelsea dakika ya 14, kabla ya mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema kuisawazishia Real Madrid dakika ya 29 sasa timu hizo zitarudiana Mei 5 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, The Blues wakihitaji hata sare ya 0-0 kwenda Fainali. Nusu Fainali nyingine ya kwanza inachezwa leo Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa baina ya wenyeji, Paris Saint-Germaine na Manchester City Saa 4:00 usiku.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA FAROUK RAMADHANI, KIPA WA ZAMANI WA SIMBA SC

Image
 

SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA DODOMA JIJI 3-1 NA KUPOTELEA ANGANI

Image
  MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuitandika Dodoma Jiji FC 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya nane na 67 na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 66, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Cleophace Mkandala dakika ya 29. Simba SC inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 25 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya watani wao jadi, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi. Dodoma Jiji yenyewe inabaki na pointi zake 38 za mechi 28 sasa katika nafasi ya sita.

YANGA SC WATUA MBEYA KWA NDEGE KUJIANDAA KUIVAA PRISONS IJUMAA KOMBE LA TFF SUMBAWANGA

Image
  KIKOSI cha Yanga kimewasili Jijini Mbeya leo kwa maandalizi ya mchezo wake wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Ijumaa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

MWADUI FC YAKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA, YAICHAPA GWAMBINA 2-1 PALE PALE MISUNGWI

Image
TIMU ya Mwadui FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza. Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Rashid Roshwa dakika ya 83 na Mohamed Hashim dakika ya 87 baada ya Gwambina kutangulia kwa bao la Meshack Abraham dakika ya 57. Mwadui FC inafikisha pointi 19 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 28, ingawa inaendelea kuzibeba timu nyingine zote 17 katika ligi hiyo ikihitaji miujiza tu kusalia msimu ujao. Gwambina yenyewe inabaki na pointi zake 30 za mechi 27 sasa katika nafasi ya 12.

BIASHARA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 NA POLISI TANZANIA YAIPIGA MTIBWA MOROGORO

Image
TIMU ya Biashara United imezinduka na kuichapa Kagera Sugar 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Mabao ya Biashara United yamefungwa na Deogratius Mafie dakika ya 24 na Lenny Kisu dakika ya 28, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 84. Kwa ushindi huo, Biashara United imefikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 28 ingawa inabaki nafasi ya nne, ikiizidi pointi nne KMC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 27 za mechi 28 ikiangukia nafasi ya 16. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imewachapa wenyeji Mtibwa Sugar 2-1 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mabao ya Polisi yamefungwa na Abdulaziz Makame dakika ya 33 na Tafiq Seif dakika ya 40, wakati la Mtibwa limefungwa na Kelvin Sabato dakika ya 51. Polisi Tanzania inafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 28 na kusogea nafasi ya nane, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 28 za mechi 27 katik

GRIEZMANN APIGA MBILI BARCELONA YASHINDA 2-1 LA LIGA

Image
MABAO ya Mfaransa Antoine Griezmann dakika za 28 na 35 jana yaliipa Barcelona ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal ambayo bao lake lilifungwa na Mnigeria Samuel Chukwueze dakika ya 26 katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Ceramica Jijini Villarreal. Kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi 71 baada ya kucheza mechi 32, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Real Madrid, wakati Atletico Madrid inaendelea kuongoza kwa pointi zake 73 za mechi.

YANGA SC 0-1 AZAM FC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

PRINCE DUBE AWAMALIZA YANGA DAKIKA ZA LALA SALAMA, AIFUNGIA BAO PEKEE AZAM FC YASHINDA 1-0 DAR

Image
  BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 86 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya vigogo, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Azam Fc imefikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 28, ingawa inabaki ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi. Mabingwa watetezi, Simba wanaendelea kutawala kileleni kwa pointi zao 58 za mechi 24.

MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA LEEDS UNITED

Image
  TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya 0-0 na Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Elland Road Elland Road, Leeds, West Yorkshire. Kwa sare hiyo, Manchester United inafikisha pointi 67 na inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi 10 na vinara, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 33. Leeds United wao wanafikisha pointi 47 katika nafasi ya tisa wakiizidi pointi moja Arsenal baada ya wote kucheza mechi 33 pia. x

MANCHESTER CITY WATWAA CARABAO YA NNE MFULULIZO ENGLAND

Image
  TIMU ya Manchester City imetwaa Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup kwa mara ya nne mfululizo kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur leo bao pekee la Aymeric Laporte dakika ya 82 Uwanja wa Wembley.