Posts
Showing posts from March, 2023
SIMBA YAKAMILISHA MAKUNDI NA KIPIGO CHA 3-1 MOROCCO
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Simba SC imekamilisha mechi zake za Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuchapwa 3-1 na wenyeji, Raja Club Athletic usiku huu Uwanja wa Mfalme Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco. Mabao ya Raja yamefungwa na mshambuliaji Mmorocco, Hamza Khabba dakika ya 44 akimalizia pasi ya kichwa ya Yousri Bouzok na ya 70 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu kwenye boksi na beki Mkenya wa Simba, Joash Onyango na Mohamed Boulacsout dakika ya 86 akimalizia pasi ya kiungo Mualgeria, Abdelraouf Benguit. Bao pekee la Simba limefungwa na mshambuliaji wake iliyemsajili dirisha dogo, Jean Bakeke dakika ya 48 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Muzamil Yassin Selemba. Kwa matokeo hayo, Raja Casablanca inafikisha pointi 16 kileleni mwa Kundi C, ikifuatiwa na Simba yenye pointi tisa na zote zimefuzu Robo Fainali zikiziacha Horoya yenye pointi saba na Vipers pointi mbili zikiishia hatua ya 16 Bora.
BILIONEA GHALIB MAZOEZINI YANGA LUBUMBASHI LEO
- Get link
- X
- Other Apps
BILIONEA Gharib Said Mohamed (katikati) akiwa na Rais wa Yanga SC, Hersi Ally Said na Makamu wake, Arafat Hajji (kulia) wakijadiliana wakati wa mazoezi ya timu leo Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tayari mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda (kishoto) aliyekuwa na timu yake ya Taifa, Chipolopolo amekwishajiunga na Yanga kuelekea mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, TP Mazembe Jumapili. Kiungo Mkongo Yanick Bangala anaonekana yuko fiti kabisa kuelekea mchezo huo dhidi ya timu ya nyumbani kwao, DRC.
MWENZA WA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI ATEMBELEA JK PARK
- Get link
- X
- Other Apps
MWENZA wa Makamu wa Rais wa Marekani Mhe.Kamalla Haris Bw. Douglas Emhoff leo Machi 30, 2023 ametembelea Kituo Cha kukuza Vipaji vya Michezo Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katika zira hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki pamoja na Mwenza wa Makamu wa Rais wa Marekani, Emhoff na kupata fursa ya kufanya ziara fupi kuona jinsi kituo hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuzungumza na vijana wanaofundishwa mpira wa Miguu na Kikapu katika Kituo hicho. Emhoff amewasihi vijana hao wajifunze kwa Ari na Bidii ili waje kuwa nyota wazuri na wakubwa Duniani. Kwa upande wake Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru Mwenza huyo kwa ziara yake katika Kituo hicho ambapo amesema ni miongoni mwa vituo vinavyolea vipaji ambavyo vinatarajiwa kuisaidia nchi katika Sekta ya michezo. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua milango kwa wadau n
MAYELE ANAWANIA KIATU CHA DHAHABU KOMBE LA CAF
- Get link
- X
- Other Apps
MSHAMBULIAJI Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele anashika nafasi ya pili katika orodha wa wafungaji wa mabao kuelekea mechi za mwisho za hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika. Fiston Mayele tayari ana mabao matatu hadi sasa akiwa nyuma ya Mghana, Paul Acquah wa Rivers United ya Nigeria na Aubin Kramo Kouamé wa ASEC ya kwao , Ivory Coast. Tayari Mayele amekwishapa Yanga SC tiketi ya Robo Fainali Ligi ya Kombe la Shirikisho kabla ya mechi za mwisho wiki di hii. Player Team G P 1st P. Acquah Rivers Utd 4 0 2 A. Kramo ASEC 4 0 2 Mostafa Fathi Pyramids 3 0 1 R. Chivaviro Gallants 3 0 0 F. Mayele Young Africans 3 0 2 B. Traoré Monastir 3 0 2 Ary Papel Akhdar 2 0 0 Z. Aloui Monastir 2 0 1
CHAMA ANAONGOZA KWA MABAO LIGI YA MABINGWA
- Get link
- X
- Other Apps
KIUNGO Mzambia wa Simba SC, Clatous Chama anaongoza kwa ufungaji wa mabao kuelekea mechi za mwisho za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi hii. Chama hadi sasa amefunga mabao manne sawa na Glody Makabi Lilepo wa Al Hilal ya Sudan na wote wana pasi mbili za mabao kila mmoja. Player Team G P 1st C. Chama Simba 4 1 2 M. Lilepo Hilal Omdurman 4 1 2 Kahraba Ahly 3 0 1 H. Khaba Raja 3 0 3 P. Shalulile Mamelodi 3 0 1 C. Mailula Mamelodi 3 0 2 J. Othos Simba 2 0 0 M. Hammouda Tunis 2 0 2 S. Benjdida Raja 2 0 1 Paulo Sérgio Merreikh 2 2 2 S. Kanouté Simba 2 0 0 Mohamed Sherif Ahly 2 0