Posts

LIPULI YAANZA VYEMA LIGI, YACHAPA MTIBWA SUGAR 3-1, MWADUI YAIPIGA 1-0 SINGIDA UNITED

Image
Na Mwandishi Wetu, IRINGA TIMU ya Lipuli FC ya Iringa imeanza vyema michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Samora mjini Iringa. Mabao ya Lipuli FC leo yamefungwa na Paul Materaz dakika ya tisa, Daruesh Salibiko dakika ya 10 wote wakimalizia pasi za Issa Ngoah na Seif Karihe dakika ya 68, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 78. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Hassan Kapalata dakika ya 25 lilitosha kuipa ushindi wa 1-0  Mwadui FC dhidi ya Singida United Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mechi za jana Kagera Sugar ya Bukoba ilishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara, mabao ya Yussuf Mhilu dakika ya 14 na Awesu Awesu dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao wenyeji walikosa penalti iliyopigwa na Jarome Lambere. Wageni Polisi Tanzania walishinda 1-0 dhidi ya Coastal Union bao pekee la Mohamed Mkopi dakika ya 33 Uw...

SIMBA SC 1-1 UD SONGO (LIGI YA MABINGWA AFRIKA)

Image

SIMBA SC YAAMBULIA SARE 1-1 NYUMBANI NA UD SONGO NA KUTOLEWA KWA BAO LA UGENINI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wametolewa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na UD Songo ya Msumbiji katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Matokeo hayo yanamaanisha UD Songo inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini, kufuatia kulazimishwa sare ya 0-0 mjini Beira wiki mbili zilizopita. Na sasa watamenyana na FC Platinum ya Zimbabwe iliyowatoa jirani zao, Big Bullets ya Malawi kwa mabao 3-2 ushindi wa ugenini jana kufuatia sare ya 0-0 nyumbani wiki mbili zilizopita.  Uwanja wa Taifa leo UD Songo waliwatangulia Simba SC kwa bao la dakika ya 14 lililofungwa na Luis Miquissone kwa shuti la mpira wa adhabu, akiutmia mwanya wa mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere kutoka kwenye kupenyeza mpira na kufunga kiulaini. Baada ya kupambana kwa muda mrefu, hatimaye Simba SC ilifanikiwa kusawazisha hilo dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti wa Nahodha wa leo, E...

CHAMA, SHEKHAN NA MAREHEMU MUSSA MSANGI ENZI ZAO SIMBA SC 2001

Image
Wachezaji wa Simba SC kutoka kulia viungo Shekhan Rashid, Athumani Jumapili ‘Chama’ na beki Mussa Msangi (sasa marehemu) kabla ya moja ya mechi zao mwaka 2001 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam

MAHOJIANO MAALIM BIN ZUBEIRY NA ISSA MANOFU

Image

AZAM FC 3-1 FASIL KENEMA (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)

Image

KMC 1-2 AS KIGALI (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)

Image