Posts

SIMBA SC 4-1 MBEYA CITY (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

GWAMBINA FC YAPAMBANIA UHAI WAKE LIGI KUU TANZANIA BARA, YAJITUTUMIA KUCHAPA DODOMA JIJI 2-0 MISUNGWI

Image
TIMU ya Gwambina FC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza. Mabao ya Gwambina FC yote yamepatikana mapema kipindi cha kwanza na yamefungwa na mshambuliaji Paul Nonga dakika ya tisa na kiungo anayechezeshwa nafasi za ulinzi pia, Gustapha Simon dakika ya 45 na ushei. Kwa ushindi huo, Gwambina FC inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 32 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 16 ikiizidi tu wastani wa mabao Coastal Union ya Tanga. Dodoma Jiji FC yenyewe inabaki na pointi zake 42 za mechi 32 sasa katika nafasi ya nane, nayo ikizidiwa tu wastani wa mabao na zote, Tanzania Prisons ya Mbeya iliyohamishia maskani Sumbawanga mkoani Rukwa na KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

RAHEEM STERLING AIPELEKA ENGLAND 16 BORA EURO 2020

Image
ENGLAND imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech usiku wa jana Uwanja wa Wembley Jijini London. Katika mchezo huo wa Kundi D, bao pekee la England limefungwa na nyota wa Manchester City, Raheem Sterling dakika ya 12 na kwa ushindi huo Three Lions inamaliza kileleni kwa pionti zake saba, mbele ya Croatia yenye pointi nne na zote zinafuzu 16 Bora. Bahati mbaya kwao Czech wamezidiwa wastani wa mabao tu na Croatia, kwani nao wamemaliza na pointi tatu, wakati Scotland imeshika mkia kwa pointi yake moja. Mechi nyingine ya mwisho ya kundi hilo jana, iliichapa Scotland 3-1 Uwanja wa Hampden Park Jijini Glasgow. Mabao ya Croatia yalifungwa na Nikola Vlasic dakika ya 17, Luka Modric dakika ya 62 na Ivan Perisic dakika ya 77, wakati la Scotland alifunga Callum William McGregor dakika ya 42.

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 UWANJA WA MKAPA

Image
 MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Mbeya City usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na Rally Bwalya dakika ya 31, Luis Miquissone dakika ya 35, Nahodha John Bocco dakika ya 47 na Clatous Chama dakika ya 86, wakati la Mbeya City limefungwa na Pastory Athanas dakika ya 51. Simba SC inafikisha pointi 73 baada ya ushindi huo katika mechi ya 29 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi. Mbeya City yenyewe baada ya kupoteza mchezo wa leo katika mechi ya 32, wanabaki na pointi zao 36 katika nafasi ya 13.

TANZANIA PRISONS YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA COASTAL UNION LEO SUMBAWANGA

Image
TANZANIA Prisons imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Samson Mbangula dakika ya 19 na Jeremiah Juma dakika ya 36, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Suleiman kwa penalti dakika ya 23 na Mudathir Said dakika ya 85. Kwa matokeo hayo Prisons inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 32 na kusogea nafasi ya saba kutoka ya tisa, wakati Coastal inafikisha pointi 34 za mechi 31 sasa, ingawa inabako nafasi ya 16 katika ligi ya timu 18 ambayo mwishoni mwa msimu tatu zitashuka.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA SEMMY KESSY MFUNGAJI BORA WA ZAMANI LIGI KUU

Image
 

AERGENTINA YANG'ARA COPA AMERICA, YAICHAPA PARAGUAY 1-0

Image
BAO pekee la kiungo wa Sevilla, Alejandro Darío Gómez dakika ya 10 jana limeipa Argentina ushindi wa 1-0 dhidi ya Paraguay katika mchezo wa Kundi A michuano ya Copa America Uwanja wa Taifa wa Brasília nchini Brazil. Argentina inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi mbili zaidi ya Chile inayofuatia baada ya wote kucheza mechi tatu. Kwa upande wao Paraguay wanabaki nafasi ya tatu na pointi zao tatu, wakifuatiwa na Uruguay pointi moja na Bolivia wanashika mkia hawana pointi.