Posts

ROBERTINHO: MPANGO TUTAKAOINGIA NAO WYDAD HAWACHOMOKI KESHO

Image
KOCHA Mbrazil wa Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ amesema kwamba wataingia mbinu nzuri kwenye mchezo kesho dhidi ya wenyeji, Wydad Athletic Club ambao utawawezesha kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba itamenyana na Wydad AC kesho Saa 3:00 usiku katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca ikihitaji sare kwenda Nusu Fainali. Hiyo inafuatia vigogo hao wa Tanzania kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Jumamosi iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. GONGA HAPA KUTAZAMA VIDEO JUMA ROBERTINHO AKIZUNGUMZA

PIGA MTONYO MREFU MERIDIANBET KASINO YA MTANDAONI

Image
Sloti   ya  Blackjack Live ​ Moja   kati   ya   michezo   pendwa   na   wengi   ni   Sloti   ya BlackJack  Live,  mchezo   huu   unapatikana   kasino   ya mtandaoni   ya  Meridianbet  ambapo   huu   unakuwa   na   karata 8  tu ,  ili   ushinde   unapaswa   utoe   karata   zisizozidi   namba  21,  lakini  pia  zikiwa   chini   ya   hapo   unaweza   kushinda   endapo karata  za  mchezeshaji   zitazidi   namba  21. Mchezo   wa   Blackjack Live   ni   mchezo   unaopend wa   na kuchezwa   sana   ulimwenguni .  Kasino   ya   mtandaoni   ya Meridianbet   inakupa   burudani   na   ushindi   kupitia   sloti   ya Blackjack Live  huku   ukiwa   na   f...

LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM UNITED 2-1 LONDON

Image
TIMU ya Liverpool jana ilitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa London. Lucas Paquetá alianza kuifungia West Ham United dakika ya 12, kabla ya Cody Gakpo kuisawazishia Liverpool dakika ya 18 na Job Joel Matip kufunga la ushindi dakika ya 67. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 32 na kusogea nafasi ya sita, wakati West Ham Unitedinabaki na pointi zake 34 za mechi 32 pia nafasi ya 14.

RIVERS UNITED 0-2 YANGA (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)

Image
 

SIMBA SC WALIPOTUA DAR KIBABE BAADA YA KUSHINDA 5-0 ZAMBIA 1979

Image
  WACHEZAJI wa Simba SC kuanzia chini kwenda juu, kipa Athumani Mambosasa (sasa marehemu), George ‘Best’ Kulagwa, Abbas Kuka, Saad Ally, Hussein Tindwa (sasa marehemu) na Hamisi Askari (marehemu pia) wakiteremka kwenye ndege baada ya kuwasili kutoka Zambia ambako waliwafunga wenyeji, Mufurila Wanderers 5-0 katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1979.  Simba SC ikafuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-4 kufuatia kufungwa 4-0 na Mufurila Wanderers Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) Dar es Salaam. Safari ya Simba iliishia raundi ya Pili ambako ilitolewa na Raccah Rovers, ikitoa sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-0 Nigeria.

DE BRUYNE APIGA MBILI MAN CITY YAITANDIKA ARSENAL 4-1

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameweka hai matumaini ya kutwaa tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu baada ya kuitandika Arsenal mabao 4-1 usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Manchester City yamefungwa na kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne mawili, dakika ya saba na 54, beki wa England John Stones dakika ya 45 na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland dakika ya 90 na ushei, wakati la Arsenal limefungwa na beki mwingine wa England, Robert Holding dakika ya 86. Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 73 katika mchezo wa 31, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakiziwa pointi mbili na Arsenal inayoendelea kuongoza Ligi ikiwa imecheza mechi mbili zaidi.

SHINDA KIRAHISI KASINO YA MTANDAONI

Image
Mawindo   yako   huenda   ukafanikiwa   kupata   chakula   pendwa kutoka   kasino   ya   mtandaoni   ya  Meridianbet,  ni   sloti   ya  Titan Dice  rahisi   kushinda   na   kucheza ,  kwa   sababu   inakupa   nafasi   ya kuchagua   kete   na   aina   ya   ushindi   unaoutaka .    Michezo   ya   Dice  ( kete )  imekuwepo   kwa   muda   mrefu   k ihistoria ,  mchezo   huu   ulianzia  China   ambapo   w aandaaji   wa   kisasa , Expanse Studios  wametengeneza   sloti   ya   Titan Dice  kukumbusha   uzuri   wa   mchezo   huu .  Kasino   ya   Mtandaoni   ya  Meridianbet   imekuletea   mchezo   huu   katika   m i kono   y ako   sasa !  Pata  ...