Posts
YANGA SC WAWASILI SALAMA DAR, WAUNGANISHA SAFARI SINGIDA
- Get link
- X
- Other Apps

KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam kikitokea Afrika Kusini ambako juzi kilikata tiketi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwatoa wenyeji, Marumo Gallants. Na baada ya kuwasili Yanga wanaunganisha safari kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars Jumapili. Yanga imeitoa Marumo Gallants ya kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini Jumatano na kwenye Fainali itakutana na USM Alger ya Algeria. Yenyewe USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani. Yanga itaanzia nyumbani katika Fainali ya kwanza Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria kwa mchezo wa marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers. Tayari Yanga wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara y...
MAWAZIRI WA MICHEZO AFRIKA MASHARIKI WAJADILIANA KUANDAA AFCON 2027
- Get link
- X
- Other Apps

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana jana Ali ongoza kikao cha Mawaziri wanaohusika na Michezo wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambao ni Peter Ongwang wa Uganda na Ababu Namwamba wa Kenya kujadili maandalizi ya pamoja ya mashindano ya Kombe la Africa Cup of Nation (AFCON) mwaka 2027. Kikao hicho ambacho kimefanyika kwa njia ya mtandao kimejadili namna nchi hizo zinavyoweza kushirikiana kuandaa mashindano hayo kupitia mashirikisho ya mipira ya nchi hizo. Mawaziri wamewasisitiza kikosi kazi kilichoteuliwa, kuandaa mpango kazi wenye ushawishi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kabla ya Mei 2023 ili nchi hizo zipate nafasi ya kuandaa mashindano hayo. Kwa upande wa Tanzania Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu @saidiyakubu1 ameshiriki pamoja na Viongozi wa Mashirikisho ya Mpira wa Miguu ya nchi hizo, ambapo kwa Tanzania imewakilishwa na Bw. Boniface Wambura kutoka Shirikis...
FAINALI EUROPA LEAGUE NI ROMA YA MOURINHO NA SEVILLA
- Get link
- X
- Other Apps

TIMU ya AS Roma imefanikiwa kutinga Fainali ya Europa League baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Bayer Leverkusen kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu leo usiku wa Alhamisi Uwanja wa BayArena Jijini Leverkusen. Timu hiyo ya kocha Mreno, José Mourinho inanufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Italia na sasa itakutana na Sevilla iliyoitoa Juventus. Sevilla imeitoa Juventus kwa jumla ya mabao 3-2 kufuatia ushindi wa 2-1 jana Hispania ikitoka kutoa droo ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Italia.
MARUMO GALLANTS 1-2 YANGA SC (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS DK SAMIA KUWAPA NDEGE YANGA KWENDA ALGERIA NA MOTISHA JUU
- Get link
- X
- Other Apps

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwapa ndege Yanga kwenda kwenye mchezo wa marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger nchini Algeria mapema mwezi ujao. Mheshimiwa Rais Dk. Samia ametoa ahadi hiyo mchana wa leo akizungumza kwenye hafla ya miaka 10 ya Azam Media Limited, Tabata Jijini Dar es Salaam. Pamoja na hilo, Rais Samia ameahidi kutoa Sh. Milioni 20 kwa kila bao ambalo Yanga watafunga kwenye michezo miwili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. “Sasa nitumie jukwaa hili hiki kuipongeza timu yetu ya Yanga, wameingia na timu yetu ya Simba, wamecheza kwenye hayo mashindano vizuri. Na niliwapa msukumo kidogo, wamefanya vizuri lakini kwa bahati moja imeishia katikati, Yanga imeendelea, nawapongeza sana,”. “Sasa Yanga inakwenda kwenye Fainali, si ndiyo? Sasa niseme yafuatayo; nilianza na mechi hizi kwa Sh. Milioni 5 kwa kila goli la ushindi, waliposogea nikasema sasa Milioni 10 kwa kila goli la ushindi, tunapo...
YANGA SC WAKIFURAHIA BAO LA MKAPA DHIDI SIMBA 1992 TAIFA
- Get link
- X
- Other Apps

WACHEZAJI wa Yanga Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu), Hamisi Gaga (marehemu), David Mwakalebela, Method Mogella (marehemu) na Abeid Mziba wakimpongeza Kenny Mkapa (kulia) baada ya kufunga bao pekee dakika ya 10 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya mtani wa jadi kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Aprili 12, mwaka 1992 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam.