Posts

IHEFU YAAMBULIA SULUHU KWA JKT TANZANIA UWANJA WA LITI

Image
WENYEJI, Ihefu SC wamelazimishwa sare ya bila mabao na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida. Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi 29 katika nafasi ya 10 na JKT Tanzania inafikisha pointi 32 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 26.  

MAKAMU RAIS WA YANGA, ARAFAT MKURUGENZI MPYA BENKI YA PBZ

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Rais Yanga SC, Arafat Ally Haji kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA GEORGE MASATU KUHUSU PAMBA KUREJEA LIGI KUU

Image
 

MTIBWA SUGAR YAZINDUKA, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 MANUNGU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Jimson Mwanuke dakika ya 15, Charles Ilamfya dakika ya 55 na Nickson Mosha dakika ya 79. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 20, ingawa inaendelea kushika mkia, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 23 nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 26.

MUDATHIR ATOKEA BENCHI KUIPA YANGA USHINDI DHIDI YA KAGERA SUGAR

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamepata ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 83 akimalizia pası ya kiungo mwenzake, Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso. Mudathir alifunga bao hilo dakika 10 tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua na kwa ushindi huo Yanga inafikisha pointi 68 katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 57 za mechi 25 na Simba SC pointi 53 za mechi 24. Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 26 pia nafasi ya saba.

MASHUJAA YAICHAPA KMC 3-0 LAKE TANGANYIKA

Image
TIMU ya Mashujaa FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Jeremanus Josephat dakika ya 12, Hassan Cheda dakika ya 22 na Relliants Lusajo dakika ya 60. Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati KMC inabaki na pointi zake 33 za mechi 26 pia nafasi ya tano katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja. Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

TABORA UNITED YAFUNGIWA KUSAJILI KWA NYINGINE TENA NA TENA

Image
KLABU ya Tabora United imefungiwa kufanya usajili wa mchezaji mpya hadi hapo itakapomlipa madai yake mchezaji wake Mkongo, Makuntima Kisombe Gulyan.