AZAM FC YAFICHUA KILICHOWAFANYA WAKATIBUA REKODI YAO
BAADA ya Mtibwa Sugar kufanikiwa kutibua rekodi ya Azam FC kuwafanya washindwe kufunga mwaka bila kupoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu, Kocha msaidizi wa Azam FC, Juma Mwambusi amefichua siri ya kushindwa kulinda rekodi yao.
Azam FC walifanikiwa kucheza michezo 16 bila kufungwa ila walipoteza mchezo wao wa 17 ambao walicheza dhidi ya Mtibwa wakiwa ugenini katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro kwa kufungwa mabao 2-0.
Mwambusi amesema wapinzani wao walitambua aina ya timu watakayokutana nayo kutokana na rekodi nzuri kwenye michezo ya nyuma waliyocheza hali iliyowafanya wabadili mbinu mara kwa mara uwanjani kutafuta matokeo na wakafanikiwa.
"Wapinzani wetu walikuwa makini katika kumaliza makosa ambayo tuliyafanya kwa kuwa mpira ni mchezo wa makosa ila tumejipanga na tumegundua tulipokosea hivyo wachezaji tutawapa mbinu mpya kutafuta ushindi.
"Tuna kazi kubwa ya kuendela kupata matokeo, kushindwa ni sehemu ya mchezo hali itakayotufanya tuzidi kuwa imara zaidi, mashabiki waendelee kutupa sapoti bado tuna nafasi ya kufanya vizuri," alisema.
Comments
Post a Comment