BIASHARA UNITED WAFUNGA MWAKA NA REKODI YAO, KUPELEKWA FIFA


BIASHARA United ya Mara ambayo imepanda Ligi Kuu msimu huu inafunga mwaka kwa rekodi ya kipekee ikiwa nafasi ya 20 kwenye msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara.

Biashara United wamekusanya pointi 10 kwenye michezo 17 waliyocheza huku wakishinda mchezo mmoja ugenini dhidi ya Singida United na wamepoteza michezo 9 na kutoa sare michezo 7 na kufanikiwa kufunga mabao 6.

Matokeo hayo yaliwafanya viongozi wa Biashara United kumpiga chini kocha wao Thiery Hitimana raia wa Rwanda ambaye amepata kibarua timu ya Ligi Daraja la Kwanza Namungo.

Hitimana ametishia kuipeleka Biashara United Shirikisho la Soka la Kimataifa 'Fifa" endapo hatalipwa stahiki zake pamoja na malimbikizo ya mshahara.

"Tumefikia maamuzi ya kuvunja mkataba lakini sijalipwa stahiki zangu, nitapeleka barua yangu TFF wakishindwa kunisaidia kudai basi nitakwenda Fifa," alisema.

Mwenyekiti wa timu hiyo Sulemani Mataso amesema watamlipa taratibu malimbikizo yake huku aliyekuwa kocha msaidizi Omary Madenge akiishika timu kwa muda.




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA