HAJI MANARA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI SIMBA 'UMMA UNAHITAJI FURAHA'
Na Haji S Manara
Wachezaji wetu wapendwa mtambue huu Umma unataka furaha tu, unawapenda na kuwathamini sana!
Nendeni kwenye shindano hili kuthibitisha ukubwa wenu na binafsi nna imani kubwa sana na nyie.
Dharau na kejeli za baadhi ya watu mzimalize uwanjani.
Kajengeni historia yenu ktk maisha ,tulikuwa wa kwanza na wa mwisho kuingia fainali ya CAF na sasa mnayo fursa ya kuifikia rekodi hiyo.
Mimi nitajitahidi kutimiza wajibu wangu wa kuhamasisha na kujuza umma wa watanzania na nyie katimizeni wajibu kwa kuweka rekodi nyingine .
Comments
Post a Comment