TFF YATOA SHUKRANI KWA SERIKALI, YATAJA MAFANIKIO HAYA


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa shukrani kwa Serikali, wadau pamoja na wanafamilia ya Mpira wa miguu kwa ushirikiano walioonyesha kwa mwaka 2018 ikiwa ni muda mchache kuweza kufunga mwaka na kuingia mwaka 2019.

Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, amesema wanaaga mwaka 2018 kwa mafanikio makubwa na wanaukaribisha mwaka 2019 huku imani ikiwa ni kufikia malengo makubwa.

"Tumechukua matajji mbalimbali 2018 ikiwa ni pamoja na lile la Ubingwa wa CECAFA na ubingwa wa COSAFA kwa kikosi cha miaka chini ya 17, Serengeti Boys, Timu ya wanawake ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens' ubingwa wa CECAFA, timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' ubingwa wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wanawake.

"Timu ya Azam FC ubingwa wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati 'Kagame' na klabu ya Simba imefanikiwa kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA