ALICHOKIANDIKA KIGWANGALLA KUHUSIANA NA PIERRE LIQUID BAADA YA KUPIGWA MKWARA NA MAKONDA
Alichokiandika Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kuhusiana na Mchekeshaji, Pierre Liquid.
Andiko hili limekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kusema wanahahabari waache kumpa kiumbele Pierre sababu ya ulevi
It’s ok! It’s ok! It’s ok, very ok kwa Pierre Liquid kufanya anachofanya na kufurahisha wanaoona ‘anachekesha’.
Nchi haiwezi kujengwa na watu wanaofanya mambo magumu magumu pekee. Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake. Pierre anatuchekesha na kutukumbusha kufurahia maisha tunapopata nafasi, haswa tunapotoka kufanya hayo mambo yetu magumu magumu!
Jamani maisha ni magumu, yana mitihani mingi na ni mafupi sana. Katika kuleta furaha na shangwe kwenye maisha ndiyo maana ‘wachekeshaji’ wakapata ajira! Wengine tusome udaktari, uhandisi na tufanye uvumbuzi na utatuzi wa changamoto na wengine watutetemeshe, watuvuruge akili, watupe raha na furaha, watuchekeshe, siku zisogee.
Maisha ndiyo haya haya! Zaidi ya yote, Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake. Tunapaswa kuulinda uhuru wa Pierre kama ambavyo Katiba ya nchi yetu inavyoelekeza. Let him be. Tumuache apate riziki yake.
Mungu anajua zaidi kwa nini hatukumjua miaka 5 iliyopita na kwa nini sasa anazua mjadala. Hata kwa mimi binafsi, Mungu anajua zaidi kwa nini sikuwa Waziri miaka mitano iliyopita, na leo ni Waziri. Mungu anatupangia maisha yetu. Anatugawia mafungu yetu.
Pengine hii inaweza kuwa sababu ya Pierre kuwa mtu bora zaidi leo kuliko ile siku aliyopiga ukelele wa raha na kubembea pale Liquid! Pengine hii ndiyo nyota yake ya jaha. Kwa hakika, Pierre atabaki kuwa juu! Pierre atabaki kuwa kileleni! Everebade sey yeeh! #HK
Comments
Post a Comment