Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM UONGOZI wa Klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji wake wa zamani, Damian Mrisho Kimti aliyefariki dunia jana jioni Jijini Dar es Salaam. Kimti alikuwa mmoja wa wachezaji ambao walicheza mchezo wa fainali ya ubingwa wa Afrika Mashariki mwaka 1992 ambao tuliibuka na ushindi dhidi ya Yanga na pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 dhidi ya Stella Abidjan. Klabu itamkumbuka Kimti kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwetu kwa kipindi chote ambacho alikuwa akichezea timu yetu. Damian Kimti (kulia) akivalishwa Medali na aliyekuwa Waziri wa Michezo, Profesa Philemon Sarungi baada ya fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 Klabu ya Simba inaungana na familia pamoja na wadau wa mpira wa miguu katika msiba huu. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Wachezaji wa Simba SC kutoka kulia Abdul Mweta, Jumanne Ucheche, Sunday Juma na Method Mogella (sasa marehemu) kabla ya moja ya mechi zao msimu wa mwaka 1990 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga kufanya usajili wa wachezaji wapya kutokana na kukiuka kanuni za bodi hiyo ya soka duniani.
Comments
Post a Comment