SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT TANZANIA LEO
Simba itashuka kwa mara ya kwanza uwanja wa Uhuru msimu huu ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 mchezo wa kwanza mbele ya JKT uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.
"Kazi kubwa kwa sasa ni kuona tunapata matokeo chanya mbele ya wapinzani wetu, tunawaheshimu na tunajua ushindani ulivyo ila hakuna namna lazima tupambane.
"Ushindani kwa sasa kwenye ligi ni mkubwa na kila timu ni bora ninaamini wachezaji wangu watapambana, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Aussems.
Comments
Post a Comment