YANGA MOTO CHINI, WAJIKITA KILELENI KIBABE, VITA YA UBINGWA YANOGA


KIKOSI cha Yanga leo kimeendeleza moto wake kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuinyoosha kwa bao 1-0 timu ya Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Azam FC iliyo chini ya Idd Cheche ilianzisha muziki kamili kwa ajili ya kuivaa Yanga ujanja ulioshtukiwa mapema na Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aliyeamua kuanza na mbinu ya kushambulia kwa kushtukiza kipindi cha kwanza.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 13 baada ya kutumia pasi ya Ibrahim Ajibu uliomshinda mlinda mlango wa Azam FC, Razack Abarola.

Mpaka dakika 90 zinakamilika hakuna mshambuliaji wa Azam aliyeweza kufumania nyavu zilizokuwa chini ya Klaus Kindoki ambaye alikuwa akilindwa vilivyo na beki Abdalah Shaibu 'Ninja'.

Ushindi wa leo unaongeza vita ya ubingwa kwa Yanga baada ya kufikisha jumla ya pointi 77 baada ya kucheza michezo 33 kwenye ligi.

Azam FC wanabaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 66 huku wakiwa na michezo mitano mkononi ili kumaliza mzunguko wa pili.

Simba inabaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 69 ikiwa imecheza michezo 27 kwenye ligi mpaka sasa.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA