YANGA SC YAENDELEZA UBABE MECHI ZA KUJIPIMA NGUVU MORO, YAICHAPA 1-0 MAWENZI

Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
YANGA SC jana imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu kwenye kambi yake Morogoro kujiandaa na msimu mpya baada ya jana kuichapa Mawenzi Marketi 1-0 Uwanja wa Jamhuri.
Bao pekee la Yanga SC katika mchezo wa jana lilifungwa na mshambuliaji mpya kutoka Rwanda, Issa Bigirimana, wakati kiungo mshambuliaji, mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi. 
Yanga SC itateremka tena dimbanki Jumapilki wiki hii kumenyana na Kariobangi Sharks ya Kenya Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Mkongwe Mrisho Ngassa akiwaongoza wenzake kuingia uwanjani jana
Kikosi cha Yanga kilichoanza jana dhidi ya Mawenzi Market na kushinda 1-0  

Mrisho Ngassa akikabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi jana Uwanja wa Jamhuri

Mechi tatu zilizotangulia Yanga ilishinda kuichapa ATN 7-0, mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana akifunga mabao matatu peke yake, huku mengine mawili yakifungwa na nyota wa Namibia, Sadney Urikhob, Mganda Juma Balinya na beki Mghana, Lamine Moro moja kila mmoja.   
Ilishinda pia 2-0 dhidi ya Moro Kids mabao ya Balinya na beki wa kulia, Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye alikosekana leo kufuatia kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania kwa maandalizi ya mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Kenya Jumapili.
Na mechi ya kwanza Yanga ilishinda 10-0, kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa akifunga mabao matatu peke yake, mengine Feisal Salum, Raphael Daudi, Mapinduzi Balama, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, Wanyarwanda Patrick Sibomana, Issa Bigirimana na Balinya, 
Na yote hayo ni maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC wakianza na Township Rollers ya Botswana kati ya Agosti 9 na 11 mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana nao mjini Gaborone kati ya Agosti 23 na 25.
Ikifanikiwa kuvuka raundi ya kwanza Yanga itakutana na mshindi kati ya Green Mamba ya Eswatini na Zesco ya Zambia.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA