MALINDI YAUNGANA NA AZAM, SIMBA, KMC NA KMKM KUAGA MAPEMA MICHUANO YA AFRIKA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Malindi SC imeungana na KMKM, zote za Zanzibar na KMC, Azam FC na Simba SC kuaga mapema michuano ya Afrika msimu kufuata jana kuchapwa 3-1 na wenyeji, Al Masry kwenye mchezo wa marudano Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrka Uwanja wa Borg El-Arab mjini Alexandria, Misri.
Matokeo hayo yanamaanisha Malindi inatupwa nje kwa jumla ya mabao ya 7-2, kufuata kufungwa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita.
Katika mchezo wa jana ambao kocha Ehab Galal aliwapumzisha wachezaji wake muhimu kufuata ushind mnono kwenye mechi ya kwanza, mabao ya Al Masry yalifungwa na Ahmed Yasser dakika ya nne na 55 na Austin Amutu dakika ya 60, wakati la Malindi lilifungwa na Ibrahim Ali dakika ya 10.

KMC ilitolewa na AS Kigali ya Rwanda Raundi ya kwanza, Azam FC imetolewa na Triangle United ya Zimbabwe Raundi ya Pili, Kombe la Shirikisho pia, KMKM ilitolewa na Primiero de Agosto ya Angola na Simba SC ilitolewa na UD Songo ya Msumbij, zote Raundi ya kwanza Lig ya Mabingwa.
Yanga SC ndio timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika lakini nayo imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zesco Unted Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa. Yanga sasa itamenyana na moja ya timu zilizovuka Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA