MECHI YA YANGA SC NA POLISI LIGI KUU YASOGEZWA MBELE KWA SIKU MOJA HADI ALHAMISI DAR

Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga SC na Polisi Tanzania umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Alhamisi na utachezwa Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo amesema hatua imefuatia ombi la Yanga wamerejea jana mjini Dar es Salaam kutoka Zambia walipokwenda kucheza na wenyeji, Zesco Unted.
Wambura amesema walipokea barua ya Yanga Septembaa 27 wakiomba mechi isogezwe mbele ili kuwapa fursa wachezaji wao waondoe uchovu wa safari ya Zamba ambako walifungwa 2-1 na Zesco United Jumamosi mjini Ndola na kukosa nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aidha, Wambura amesema mchezo mwingine pia dhidi ya Coastal Union uliokuwa uchezwe Oktoba 5 na umesogezwa mbeke kwa siku moja kwa sababu Uwanja wa Uhuru utakuwa na matumizi mengine ya kijamii siku hiyo.
Lakini Wambura amewaambia Yanga SC kwamba ahueni hiyo ni ya mwisho na kwamba kuanzia sasa hawatakuwa tayati kupangua tena ratiba ya Ligi Kuu.
“Wanapopanga safari zao lazima wazingatie ratiba ya Ligi Kuu, mechi sasa ni Oktoba 3 na ile dhidi ya Coastal Union ni Oktoba 6 badala ya Oktoba 5. Kwa vile Oktoba 5 Uwanja wa Uhuru utakuwa na matumizi mengine ya kijamii, hivyo imekuwa nafuu kwa Yanga,”amesema Wambura.
Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema kwamba sababu kubwa ya kuomba Bodi ya Ligi kutokana na kupata muda wa wachezaji kupumzika.
"Sababu kubwa ni kutokana na wachezaji watakuwa wanechoka na safari, kwani timu inarudi Leo saa moja usiku na kufanya mazoezi siku ya Kesho na jumatano kucheza mechi,".
"Tumeomba ili tupate siku moja wachezaji kupata mapumziko na kufanya mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Polisi Tanzania," alisema Mwakalebela.
Kwa kufungwa 2-1 na Zesco United, Yanga inatolewa kwa jumla ya mabao 3-2, kufuatia sare ya 1-1 baina ya timu hizo kwenye mchezo wa kwanza Septemba 14 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na sasa itamenyana na moja ya timu zilizovuka Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo mingine ya CAF.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA