TANZANIA BARA YAIPIGA UGANDA 4-2, KUIVAA TENA KENYA NUSU FAINALI CECAFA U20

Na Mwandishi Wetu, GULU
TIMU ya Tanzania Bara imefanikiwa kuingia Nusu Fanali ya michuano ya Kombe la Matafa ya Afrika Masharki na Kati (CECAFA Challenge U20) baada ya ushind wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Uganda jioni Uwanja wa Kumbukumbu wa Gulu.
Mabao ya Tanzania Bara leo yamefungwa na washambuliaji wake hodari, Andrew Albert Simchimba dakika za 25 na 62 na Kelvin Pius John ‘Mbappe’ dakika za 89 na 90 na ushe, wakati ya Uganda yamefungwa na Aziz Kayondo dakika ya 46 na 76. 
Robo Fainali nyingine Sudan imefunga 1-0 Sudan Kusini Uwanja wa Gulu pia, Kenya imefunga Burundi 2-1 na Eritrea imeiadhibu 5-0 Zanzibar Uwanja wa Njeru.


Sasa Tanzania Bara itamenyana na Kenya katika Nusu Fainali Jumanne yakiwa ni marudio ya mchezo wa Kundi B ulioisha kwa sare ya 2-2 na Ertrea itamenyana na Sudan, wakati Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA