HASSAN MWAKINYO AMSHINDA KWA POINTI MFILIPINO, KIDUKU AMMALIZA ‘MSAUZI’ KWA TKO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BONDIA Mtanzania, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kutetea taji lake la UBO International uzito wa Super Welter baada ya kumshinda Mfilipino, Arnel Tinampay kwa pointi katika pambano la raundi 10 usiku wa jana Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Jaji wa kwanza alitoa pointi 97-93, wa pili akatoa 98-92 wote wakimpa mshindi bondia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 24 na wa tatu akatoa 96-96 kwa maana ya sare.
Hilo linakuwa pambano la 16 kwa Mwakinyo kushinda kati ya 18, mengi mawili akipoteza tangu aanze ngumi za kulipwa miaka minne iliyopita pambano lake la kwanza akimshinda Alibaba Ramadhani kwa pointi ukumbi wa Tangamano, Tanga Novemba 29, mwaka 2015.




Katika mapambano ya utangulizi, Twaha Kassim Rubaha ‘Twaha Kiduku’ alipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kufanikiwa kumshinda France Ramabolu wa Afrika Kusini kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya tatu uzito wa Super Welter pia.
Na katika pambano baina ya wapinzani wa kitongoji kimoja, Mabibo na walioibukia katika gym moja, Mfaume Mfaume aliibuka mbabe wa Keisi Ally kwa ushindi wa pointi za majaji wote pambano la raundi nane uzito wa Welter.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA