JONAS MKUDE AUNGANISHWA NA MORRISON KESI YA KUPIGA ‘VIWIKO’ KAMATI YA NIDHAMU TFF

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Februari 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kwa Vyombo vya Habari leo mjini Dar es Salaam imesema kwamba Mkude alimpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United FC, Ally Kombo katika mchezo wa Ligi Kuu ambao timu yake, Simba SC ilishinda 3-1.
Hata hivyo, kiungo huyo aliyecheza vizuri siku hiyo, Mkude alinaswa na picha za Televisheni akimpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United, Ally Kombo.

Lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania alikuwa mwenye bahati kwa sababu marefa hawakuona tukio hilo, hivyo kuepuka adhabu ya kadi mchezoni.    
Mkude anaungana na kiungo wa mahasimu wao wa jadi, Yanga SC, Mghana Bernard Morrison kwenda kusimama Kamati ya Nidhamu – wote kwa makosa yanayofanana, kupiga kiwiko.
Morrison yeye alimpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa pia.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA