KASEJA AJIFUA KWA BIDII BAADA YA KUPONA GOTI ILI AREJESHWE TAIFA STARS AKACHEZE CHAN

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIPA mkongwe nchini, Juma Kaseja amesema kwamba atapambana kurejesha kiwango chake baada ya kupona maumivu ya goti ili awe fiti na kurejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajil ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
“Nitapambana, nitarejesha kiwango, na ninaamini nitakuwemo kwenye timu,” amesema Kaseja ambaye kwa sasa anadakia klabu ya KMC, baada ya kudakia, Moro United, Simba, Yanga, Mbeya City na Kagera Sugar.
Juma Kaseja amesema anaamini kikosi kipya cha Taifa Stars kitakachoitwa kwa ajili ya michuano ya CHAN na yeye atakuwemo kwa kuwa ameshapona jeraha lake na sasa anarejea kwenye mapambano ya kuwania namba, asema KMC haijaanguka.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kwa ugonjwa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Mechi zilizofutwa ni za tatu za na za nne kufuzu Fainali za AFCON 2021 ambazo zilipangwa kufanyika kati ya Machi 25 na 31 mwaka huu, kufuzu Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake chini ya umri wa miaka 20 zilizopangwa kufanyika kati ya Machi 20 na 22 na marudiano Machi 27 na 29 mwaka huu.
Aidha, CAF pia imesitisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa (AFCON) kwa Wanawake 2020 zilizopangwa kufanyika kati ya Aprili 8 na 14 mwaka 2020 – na ratiba mpya ya michuano hiyo itatangazwa kwa wakati.
Kaseja ndiye kipa aliyeidakia Taifa Stars katika mechi za kufuzu CHAN ikizitoa Kenya na Sudan na kupata tiketi ya kucheza fainali za michuano hiyo kwa mara ya pili tu kihistoria baada ya zile za kwanza kabisa mwaka 2009 nchini Ivory Coast. 
Kaseja pa alikuwa kipa wa Taifa Stars ikiitoa Burundi kwa mikwaju ya penalti na kufuzu hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe ka Dunia 2022 Qatar.
Hata hivyo, baada ya mafanikio hayo akajikuta anaenguliwa kikosini kutoakana na maumivu ya goti yaliyomsababisha afanyiwe upasuaji wa goti Desemba 28 mwaka jana.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA