TIMU YA TAIFA YA KARATE TANZANIA YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA JAPAN OKTOBA

Na Mwandishi Wetum DAR ES SALAAM
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate imepata Nafasi ya kwenda  kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Karate yatakayofaanyika nchini Japan Oktoba mwaka huu.
Mashindano hayo ya Karate ya Dunia huwa yanafanyika kila baada ya miaka mitatu na kwa mwaka huu Tanzania pia imepata nafasi ya kipekee kwa kutoa Jaji wa michuano hiyo ambaye ni Sensei Jerome Mhagama.
BBC Imezungumza Jerome Muhagama ambaye Pia ni  Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzania Juu ya nafasi hiyo iliyopata nchi ya Tanzania.
Sensei Jerome Mhagama (kushoto) atakuwa Jaji katika mashindano ya Dunia ya Karate Japan Oktoba mwaka huu 

Haya ni mashindano ya 15 ya Dunia Tangu kuanzishwa kwake,na Tanzania imewahi kushirikiki mara Mbili katika mashindano hayo. Kwa mara ya kwanza mwaka 2011 mashindano hayo yaliyofanyika Nchini Tailand,Tanzania Ilipeleka mchezaji mmoja ambaye alifika katika hatua ya 16 Bora.
Mwaka 2014 Katika mashindano yaliyofanyika Japan Tanzania Ilishiriki katika mashindano hayo kwa Kupeleka Jaji.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA