Posts

Showing posts from May, 2020

YANGA SC WALIVYOSAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA KAMPUNI YA LA LIGA KUPITIA KLABU YA SEVILLA

Image
Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla (kushoto) akisaini mkataba wa ushirikiano na Kampuni ya La Liga kupitia klabu ya Sevilla ya Hispania leo hoteli ya Serena Jijini Dares Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM wanaosimamia zoezi hilo kwa gharama zao, Hersi Said na wanaoshuhudia ni wanasheria wa pande zote mbili (Yanga na GSM). Zoezi hilo lilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete

NYOTA WA SIMBA 1992, BAKARI IDDI, MAGOSO NA MAREHEMU GEBO PETER

Image
WACHEZAJI wa Simba SC kutoka kulia kiungo mshambuliaji Bakari Iddi, beki Fikiri Magoso na mshambuliaji Gabriel ‘Gebo’ Peter Magali (sasa marehemu) kabla ya moja ya mechi zao za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1992 Uwanja wa Amaan, Zanzibar, msimu ambao Wekundu hao wa Msimbazi walibeba taji hilo baada ya kuwafunga watani, Yanga kwa penalti kwenye fainali.

BEKI MKONGWE, SALUM KANONI KUPELA AKIWAONGOZA WACHEZAJI WENZAKE MTIBWA SUGAR MAZOEZINI MANUNGU

Image
Beki mkongwe wa Mtibwa Sugar, Salum Kanoni Kupela akikokota mpira mazoezini Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro kujiandaa kumalizia msimu baada ya zuio la tangu katikati ya Machi kwa hofu ya mambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

MBWANA SAMATTA AFICHUA; “UMALIZIAJI AU KULENGA SHABAHA NDIYO ZOEZI NINALOLIPENDA ZAIDI”

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba anapenda zaidi kujifunza kufunga mabao kuliko aina nyingine yoyote ya mazoezi. Samatta ameposti picha akiwa mazoezini na klabu yake, Aston Villa, Uwanja wa Bodymoor Heath na kuambatanisha na ujumbe; “Zoezi la umaliziaji au kulenga shabaha ndiyo zoezi ninalolipenda zaidi,”. Samatta anatarajiwa kuwa mfungaji mpya tishio barani Ulaya na hiyo ni baada ya bao alilofunga akiwa KRC Genk ya Ubelgji dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Novemba 5, 2019 Uwanja wa Anfield kuteuliwa Bao Bora la Msimu na klabu yake hiyo ya zamani iliyochapwa 2-1 siku hiyo. Ni Januari tu mwaka huu KRC Genk ilimuuza Mbwana Samatta klabu ya Aston Villa baada ya kuwa naye tangu Januari 2016 ilipomnunua TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).  Samatta aliyekuwa anacheza Anfield kwa mara ya kwanza usiku wa Novemba 5 mwaka jana, aliifungia KRC Genk bao hilo dakika ya 40 kwa kichwa a

NI MZIGO MZITO CHRISTIAN BELLA ANABEBESHWA, AACHWE AFANYE MAMBO KWA MASLAHI YAKE

Image
NAKUMBUKA wakati ajali ya MV Bukoba ilipotokea mwaka 1996 na kukatisha uhai wa mamia ya Watanzania, nilipata kumshuhudia mmoja wa waombolezaji ambaye aliniacha kinywa wazi. Muombolezaji yule aliyepoteza mtoto wake wa kiume kwenye ajali ile, alikuwa analalamika kwanini mwanaye amefariki, kwanini hakuwa mmoja kati ya watu waliosalimika, kwanini basi hawakufariki watu wote, kwanini wengine wafe halafu wengine wasalimike. Pamoja na kutambua kwangu kuwa mara nyingi wafiwa hushikwa na kiwewe hadi hata kumkufuru Mungu, lakini lile la mfiwa kutaka watu wote wafariki kwenye ajali liliniduwaza sana. Hali hii ipo pia kwenye muziki wa Dansi ambao umeyumba kidogo sokoni ambapo wale wanaoonekana kufanikiwa kuokoka kwenye anguko la soko la muziki huo, wananyooshewa kidole pamoja na kutazamwa kwa jicho la kwanini. Christian Bella, mwimbaji wa dansi anayetusua vizuri sokoni, amekuwa mlengwa mkuu, anakumbana na maneno makali kutoka kwa wadau na mashabiki wa muziki wa Dansi. Bella pengine kwa kuta

MAMBO YA KUZINGATIA MICHEZONI WAKATI WA MAAMBUKIZI YA CORONA

Image
Na Mwandishi Wetu, DODOMA UTANGULIZI; Kufuatia kuwepo kwa ugonjwa wa CoVID-19 unaotokana na Virusi vya Corona nchini ambao uliripotiwa kwa mara ya kwanza mwezi Machi, 2020, Serikali iliamua kusimamisha shughuli zote za michezo ikiwemo mashindano ya Ligi za Soka kwa lengo la kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo. Takwimu za mwenendo wa ugonjwa wa CoVID-19 nchini kwa sasa zinaonesha kupungua kwa wagonjwa jambo ambalo linaleta matumaini ya kuendelea na shughuli za kijamii ikiwemo Serikali kupitia kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuruhusu shughuli za michezo kuendelea kuanzia Juni Mosi, 2020. Aidha, Mhe. Rais aliziagiza Wizara zenye dhamana ya Afya na ile ya Michezo kuandaa Mwongozo wa pamoja wa namna michezo itakavyorejea nchini hususani ligi za soka. Kwa maelekezo hayo, wataalamu na baadaye viongozi wa sekta hizi mbili, kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa michezo yakiwemo mabaraza, shirikisho, vyama na vilabu vyenyewe, wamekubaliana kuzingatiwa. Mambo ya Kuzingatia; Utaratibu huu unale

SIMBA NA YANGA ZINAWEZA KUKUTANA TENA NUSU FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM VIGOGO, Simba na Yanga wanaweza kukutana kwa mara ya tatu msimu iwapo watavuka hatua ya Robo ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC). Hiyo ni baada ya ratiba ya Robo Fainali na Nusu Fainali ya michuano hiyo kupangwa leo katika studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo zilizopo Tabata Jijini Dar es Salaam.  Simba SC watakutana na mabingwa watetezi, Azam FC na Yanga SC watamenyana na Kagera Sugar katika Robo Fainali wote wakiwa nyumbani na vigogo hao wakishinda watakutana baina yao kwenye Nusu Fainali. Robo Fainali nyingine zitakuwa ni kati ya Namungo FC dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na Sahare All Stars dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na washindi wa mechi hizo watakutana Nusu Fainali. Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto aliyeongoza droo hiyo akisaidiwa na wachezaji wa zamani, beki wa zamani wa Simba SC Boniphace Paw

MECHI ZOTE ZILIZOSALIA ZA LIGI KUU TANZANIA BARA KUCHEZWA NYUMBANI NA UGENINI KUANZIA JUNI 13

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MECHI zilizosalia za Ligi Kuu ya Tanzania Bara itachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini kuanzia Juni 13, mwaka huu kama kawaida tofauti na tamko la awali la Serikali kwamba itachezwa kwa vituo. Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema leo Jijini Dar es Salaam kwamba maazimio hayo waliyafikia jana kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi na kuyafikisha Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kasongo alisema ratiba nzima ya mechi zilizosalia za Ligi Kuu ya Tanzania itatolewa Jumapili ingawa hakusema kama mashabiki wataruhusiwa au la. Awali Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alisema mechi zilizosalia za Ligi Kuu zichezwe Dar es Salaam pekee katika viwanja vya Taifa, Uhuru na Azam Complex pamoja na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) iliyofikia hatua ya robo Fainali. Kuhusu mechi za Ligi Daraja la Kwanza na la Pili, Waziri Mwakyembe alisema kwamba

JEZI MPYA ZA MSIMU UJAO ZA MANCHESTER UNITED ZIMEVUJA, HIZI HAPA

Image
Jezi mpya za msimu ujao, 2020-21 za Manchester United zimevuja kwenye mitandao kama unavyoweza kujonea, vipi ni nzuri? PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MAFUNDI JONAS MKUDE, DEO KANDA NA NYOA WENGINE MAZEOZINI JANA SIMBA SC IKIJIANDAA KUMALIZIA SHUGHULI

Image
Viungo wa Simba SC, Jonas Mkude (kushoto) na Mkongo Deo Kanda (kula) wakikimbia jana Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam katika siku ya kwanza ya timu yao kurejea mazoezini  kujiandaa kumalizia msimu baada ya zuio la tangu katikati ya Machi kwa hofu ya mambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19 Viungo wa Simba SC, Said Ndemla (kulia) na Shiza Kichuya (kushoto) wakikimbia mazoezini Nahodha wa Simba SC, mshambulaji John Raphael Bocco akiwa mazoezini jana Bunju Beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni akiwa mazoezini jana

KAPTENI PAPY KABAMBA TSHISHIMBI ALIVYOWAONGOZA WACHEZAJI WENZAKE YANGA MAZOEZINI JANA DAR

Image
Nahodha wa Yanga, kiungo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi (kushoto) akikimbia na beki Ali Ahmad Ali  jana katika siku ya kwanza ya timu yake kurejea mazoezini  kujiandaa kumalizia msimu baada ya zuio la tangu katikati ya Machi kwa hofu ya mambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19 Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akitoa maelekezo kwa wachezaji jana  Wachezaji wa Yanga wakijivuta mazoezini jana Jijini Dar es Salaam

AZAM FC WALIVYOREJEA MAZOEZINI JANA CHAMAZI KUJIANDAA KUMALIZIA MSIMU

Image
Mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda akikokota mpira jana katika siku ya kwanza ya timu yake kurejea mazoezini  kujiandaa kumalizia msimu baada ya zuio la tangu katikati ya Machi kwa hofu ya mambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19 Kiungo wa Azam FC, Iddi Suleiman Nado akikokota mpira jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam   Kiungo wa Azam FC, Frank Raymond Domayo akichezea mpira jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam  Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' akikimbia mazoezini wanja wa Azam Complex jana

BARCELONA YATUMIA JANGA LA CORONA KUJIONGEZEA PATO KWA KUUZA BARAKOA

Image
KLABU ya Barcelona imekitumia kwa manufaa kipindi cha maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19 kwa kutoa Barakoa za aina tatu na kuingiza kwenye soko la bidhaa zake kila moja ikiuzwa kwa Pauni 16   PICHA ZAID GONGA HAPA

WACHEZAJI WA SIMBA SC WAFANYIWA VIPIMO MBALIMBALI KABLA YA KUANZA MAZOEZI LEO KUJIANDAA KUMALIZIA MSIMU

Image
Daktari akimpima beki wa Simba SC leo tayari kuanza mazoezi kujiandaa kumalizia msimu baada ya zuio la tangu katikati ya Machi kwa hofu ya mambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19 Beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' (kulia) akipima uzito huku akishuhudiwa na mchezaji mwenzake, kiungo Said Ndemla

WACHEZAJI YANGA SC WALIPOPIMWA CORONA JANA TAYARI KUANZA MAZOEZI KUJIANDAA KUMALIZIA LIGI KUU

Image
Daktari wa Yanga SC, Shecky Mngazija (kushoto) akiwapima wachezaji wa timu hiyo jana tayari kuanza mazoezi kujiandaa kumalizia msimu baada ya zuio la tangu katikati ya Machi kwa hofu ya mambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

KOCHA MRUNDI KUANZA KUINOA AZAM FC KUJIANDAA KUMALIZIA MSIMU WA LIGI KUU

Image
Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Mrundi Bahati Vivier, tayari yupo nchini kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo, inayoanza mazoezi rasmi leo Jumatano, kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobakia za msimu huu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Vivier ambaye atakuwa sambamba na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar, anaanza kukinoa kikosi hicho akisubiria kurejea nchini kwa Kocha Mkuu, Aristica Cioaba na Kocha wa Viungo, Costel Birsan, waliokwama nchini kwao, Romania. Makocha hao wanasubiria kurejea kwa usafiri wa ndege katika anga la Ulaya mwezi ujao, kufuatia makampuni mengi ya usafiri wa anga kusimamisha shughuli zao baada ya mlipuko wa virusi vya Corona (COVID-19).  Mrundi Bahati Vivier anatarajiwa kuanza kuinoa Azam FC leo kujiandaa kumalizia msimu Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa pamoja itaendelea kuanzia Juni baada ya kusimama tangu Machi 17, mwaka huu kwa agizo la Waziri Mkuu, Kassim

BAYERN MUNICH YAICHAPA BORUSSIA DORTMUND 1-0 NA KUKARIBIA TAJI LA NANE MFULULIZO BUNDESLIGA

Image
Joshua Kimmich akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich bao pekee dakika ya 43 ikiwalaza wenyeji, Borussia Dortmund 1-0 kwenye mchezo wa Bundesliga Uwanja wa Signal-Iduna-Park Jijini Dortmund jana. Ushindi huo unawafanya Bayern Munich waongoze Bundesliga kwa pointi saba zaidi ya Dortmund zikiwa zimesala mechi sita hivyo kukaribia kutwaa taji la nane mfululizo la ligi hiyo   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

PAMOJA NA KUREJEA, CRISTIANO RONALDO AFANYA MAZOEZI YA PEKE YAKE JUVUNTUS

Image
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi pembeni ya wachezaji wenzake wa Juventus baada ya kurejea kufuatia mapumziko ya tangu katikati ya Machi kwa hofu ya maambukizi ya virusi vya corona   PICHA ZAIDI GONGA HAPA