SIMBA SC YATWAA TAJI LA TATU MFULULIZO LIGI KUU BAADA YA SARE YA 0-0 NA PRISONS SOKOINE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC wamefanikiwa kutwaa taji la tatu mfululizo la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Tanzania Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa sare hiyo, Simba SC wanafikisha pointi 79 baada ya kucheza mechi 32, wakiwaacha mbali watani wao wa jadi, Yanga SC wanaofuatia katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 32 pia.  
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Abubakar Mturo aliyesaidiwa na Janeth Balama na Paschal Joseph, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na sifa ziwaendee makipa Aishi Manula wa Simba na Jeremiah Kasubi wa TZ Prsions kwa kazi nzuri ya kuokoa michomo langoni.
Hilo linakuwa taji la 21 la Ligi Kuu kwa Simba SC baada ya awali kubeba taji hilo katika misimu ya 1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007 (Ligi Ndogo), 2010, 2012, 2018 na 2019.
Vigogo, Yanga SC wanabaki kuwa mabingwa mara nyingi zaidi wa taji hilo, 26 katika misimu ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 2015, 2016 na 2017.
Timu nyingine zilizobeba taji hilo ni Cosmopolitans ya Dar es Salaam 1967, Mseto SC ya Morogoro 1975, Pan African ya Dar es Salaam 1982, Tukuyu Stars ya Mbeya 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, Mtibwa Sugar ya Morogoro 1999 na 2000 na Azam FC 2014.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbao FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, bao pekee la Waziri Junior dakika ya 65 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. 
Kikosi cha Tanzania Prisons kilikuwa; Jeremiah Kisubi, Michael Ismail, Benjamin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya/Ismail Azizi dk61, Ezekia Mwashilindi, Samson Mbangula, Jeremiah Juma na Adil Buha. 
Simba SC; Aishi Manula, Haruna Shamte, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Kennedyy Juma, Gerson Fraga, Hassan Dilunga/Luis Miquissone dk67, Muzamil Yassin, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu/Clatous Chama dk46 na Mraj Athumani ‘Madenge’/John Bocco dk80.
Yanga SC iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1974 chini ya kocha Tambwe Leya na magwiji kama Sunday Manara na Gibson Sembuli (marehemu)

MABINGWA WA JUMLA LIGI KUU:
1965 - Sunderland (Dar es Salaam)
1966 - Sunderland (Dar es Salaam)
1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam) 
1968 : Yanga 
1969 : Yanga 
1970 : Yanga 
1971 : Yanga 
1972 : Simba 
1973 : Simba 
1974 : Yanga 
1975 : Mseto SC (Morogoro) 
1976 : Simba 
1977 : Simba 
1978 : Simba 
1979 : Simba 
1980 : Simba 
1981 : Yanga 
1982 : Pan African 
1983 : Yanga 
1984 : Simba 
1985 : Yanga 
1986 : Tukuyu Stars (Mbeya) 
1987 : Yanga 
1988 : Coastal Union (Tanga) 
1989 : Yanga 
1990 : Simba  
1991 : Yanga 
1992 : Yanga 
1993 : Yanga 
1994 : Simba 
1995 : Simba 
1996 : Yanga 
1997 : Yanga 
1998 : Yanga 
1999 : Mtibwa Sugar (Morogoro) 
2000 : Mtibwa Sugar (Morogoro)  
2001 : Simba 
2002 : Yanga 
2003 : Simba 
2004 : Simba 
2005 : Yanga 
2006 : Yanga 
2007 : Simba (Ligi Ndogo) 
2008 : Yanga 
2009:  Yanga 
2010: Simba SC
2011: Yanga SC
2012: Simba SC
2013: Yanga SC
2014: Azam FC
2015; Yanga SC
2016: Yanga SC
2017: Yanga SC
2018: Simba SC
2019: Simba SC
2020: Simba SC


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA