Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA wa Tanzania, Simba Sports Club wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 31, kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kuwahadaa viungo wa Ahly Aliou Dieng, raia wa Mali na Mmisri Akram Tawfik kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama. Kwa ushindi huo, Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili kufuatia ushindi wa ugenini wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AS Vita mjini Kinshasa Febaruari 12. Baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, E l Merreikh leo Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakaa nafasi ya pili ikilingana pointi na Al Ahly. Mechi ijayo S