HATIMAYE MO DEWJI AKABIDHI HUNDI YA SH BILIONI 20 KUNUNUA ASILIMIA 49 YA HISA NDANI YA KLABU YA SIMBA


HATIMAYE mfanyabiashara, Mohamed Gulam Dewji amekabidhi hundi ya Sh. Bilioni 20 kununua hisa asilimia 49 za klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
Mo Dewji amemkabidhi hundi hiyo Mwenyekiti wa klabu, Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Ally Mangungu mchana wa leo katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Golden Jubilee Jijini Dar es Salaam.
"Tumekamilisha mchakato wa mabadiliko. Tumepata hati kutoka FCC ya kuturuhusu kumalizia mchakato," amesema Mo Dewji na kuongeza; "Leo naweka hiyo Bilioni 20 ya hisa asilimia 49 mbele ya mdhamini wa klabu na mwenyekiti wa klabu,".
Mo Dewji amesema ndani ya miaka minne tangu mchakato huo umeanza amekuwa akiihudumia Simba kwa kila kitu na katika kipindi hicho chote ametumia kiasi cha Sh. Bilioni 21.3, wastani wa Bilioni 5.3 kwa mwaka kwa ajili ya usajili wa wachezaji, makocha, maandalizi ya kabla ya msimu, mishahara na uendeshaji wa klabu,". 
Mo amefurahi uwejezaji wake umekuwa na tija, kwani klabu imeshinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili.
Mfanyabiashra huyo aliyeanza kuifadhili Simba tangu 1998 hadi 2005 kabla ya kujitoa na kurejea miaka minne iliyopita, amesema hamu yake kubwa kwa sasa ni kushinda ubingwa wa Afrika.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA