MTIBWA SUGAR YAIFUMUA TRANSIT CAMP 4-1 NA COASTAL UNION YALAZIMISHA SARE YA 2-2 NA PAMBA JIJINI MWANZA MECHI ZA KWANZA ZA PLAY-OFFS

TIMU za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Coastal Union ya Tanga zimejiweka katika nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya mechi za kwanza za mchujo leo ugenini dhidi ya timu za Daraja la Kwanza.
Mtibwa Sugar, mabingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo 1999 na 2000 wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Transit Camp Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ibrahim Ahmada Hilika matatu dakika za nane 69 na 85 na Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 12, wakati la Transit Camp limefungwa na Wanzanga Karegea dakika ya15.




Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Ibrahim Ahmada Hilika akikabidhiwa mpira baada ya mechi kufuatia kufunga mabao matatu 'hat trick'

Nayo Pamba imelazimishwa sare ya 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, tena wenyeji hao wakipoteza mkwaju wa penalti mapema kipindi cha kwanza uliopigwa na Elinywesia Edward dakika ya nne.
Mabao ya Pamba yalifungwa na James Ambroce dakika ya 12 na Haule dakika ya 77 na ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Suleiman dakika ya kwanza na Raizin Hafidh dakika ya 88.
Mechi za marudiano zitachezwa Jumamosi, Mtibwa na Transit Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Coastal na Pamba Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Baada ya JKT Tanzania, Gwambina, Ihefu na Mwadui FC kushuka, Mtibwa na Coastal zikaangukia kwenye Play-Offs dhidi ya timu hizo za FDL kuwania kubaki Ligi Kuu.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA