MO DEWJI AJIUZULU UENYEKITI SIMBA SC

BILIONEA mwenye asili ya Kiasia, Mohamed ‘Mo Dewji’ ametangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Simba SC na kubaki mwekezaji pekee kwa umiliki wa asilimia 49 ya hisa zenye thamani ya Sh. Bilioni 20.
Akitangaza uamuzi wake huo leo, Dewji amesema kwamba nafasi yake itashikiliwa na aliyekuwa Makamu wake, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’.
"Muda umefika mimi kama Mohamed, tumefanya mkutano tarehe 21 mwezi wa tisa, 2021 na tumekubaliana kwamba mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Simba Sports Club,". 



"Naomba sana wana Simba msifikirie mimi nimeondoka kwenye Simba, bali bado ni mwekezaji kwenye Simba ni mwana hisa kwenye Simba, naipenda Simba na nitaendelea kuipenda Simba mpaka siku yangu ya mwisho," amesema Dewji leo Dares Salaam.
Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya timu kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Biashara United katika mchezo wake wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara huku Nahodha, John Bocco akikosa penalti dakika ya 90.  
Januari 13 mwaka 2020 Mo pia alitangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo na kubaki kama mwekezaji mara tu baada ya baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi uliomalizika kwa Simba SC kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kama ilivyokuwa mwaka jana, Mo Dewji alijiuzulu baada ya Simba SC kufungwa kwenye fainali ya Kombe la Kombe la Mapinduzi na safari hii anang'atuka timu ikitoka kutoa sare na Biashara na kufungwa na taini Yanva 1-0 katia Ngao yaJmii.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA