Posts
Showing posts from December, 2021
YANGA YAUAGA MWAKA KWA USHINDI WA 4-0
- Get link
- X
- Other Apps
VINARA, Yanga SC wamefunga mwaka ushindi wa kishindo wa 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkala Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Wakongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 42, Jesus Ducapel Moloko dakika ya 57, Justin Billary aliyejifunga dakika ya 71 na kiungo Mganda dakika ya 81. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 11, nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC wanaofuatia ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi. Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao 16 za mechi 11 pia katika nafasi ya sita.
MAN UNITED YAICHAPA BURNLEY 3-0 OLD TRAFFORD
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Scott McTominay dakika ya nane, Ben Mee aliyejifunga dakika ya 27 katika harakati za kuokoa krosi ya Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo aliyekamilishwa shangwe za ushindi dakika ya 35. Kwa ushindi huo, Manchester United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya sita, wakati Burnley inabaki na pointi zake 11 za mechi 16 sasa katika nafasi ya 18.
CHARLES HILLARY ATEULIWA MKURUGENZI MAWASILIANO IKULU ZENJI
- Get link
- X
- Other Apps
NAMUNGO FC YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA BIASHARA
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi. Namungo FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake tegemeo, Relliant Lusajo dakika ya 10, kabla ya Dennis Nkane kuisawazishia Biashara United dakika 37. Kwa sare hiyo kwenye mchezo wa 11 kwa wote, Namungo FC wanafikisha pointi 13 katika nafasi ya nane, wakati Biashara wanafikisha pointi tisa katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
YANGA YATAJA VIINGILIO KESHO MECHI NA DODOMA JIJI
- Get link
- X
- Other Apps
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga SC na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh.5,000. Katika hatua nyingine, klabu ya Yanga imerahisisha njia za wapenzi wake kujisajili kuwa wanachama na sasa wanaenda kufanya zoezi hilo kupitia simu zao.
AFCON 2021 LIVE STARTIMES
- Get link
- X
- Other Apps
KAMPUNI ya Star Media (T) Limited kupitia chapa yake ya Startimes imethibitisha kushirikiana na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuonyesha LIVE kombe la mataifa ya Africa 2021(AFCON 2021). AFCON 21 itapigwa nchini Cameroon, Startimes imepata haki za matangazo kurusha michezo yote 52 ya michuano hii, yaani kuanzia tarehe 9 Januari 2022 mpaka Februari 6, 2022.Timu kuu shiriki ni pamoja na Senegal, Misri, Morocco, Tunisia, wenyeji Cameroon, Ivory Coast, Ghana na mabingwa watetezi Algeria. StarTimes itarusha michezo hii kupitia chaneli za michezo za ST. World Football (Kiingereza), Sports Premium (Kifaransa) pamoja na TV3 kwa Lugha ya Kiswahili. Ili kuweza kutazama michezo hii moja kwa moja lipia kifurushi chako cha Mwezi cha Dish (Smart) Tsh 21,000 na Antenna (Uhuru) Tsh 20,000.
MAN CITY YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA MWINGINE
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA watetezi, Manchester City wamezidi kuwaacha mbali wapinzani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford City usiku wa Jumatano Uwanja wa Brentford Community, Brentford, Middlesex. Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, Phil Foden dakika ya 16 akimalizia kazi nzuri ya Kevin de Bruyne kumchambua kipa Alvaro Fernandez. Ushindi huo unaifanya Manchester City imalize mwaka kileleni mwa Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 50, nane zaidi ya mabingwa wa Ulaya, Chelsea wanaofuatia baada ya wote kucheza mechi 20. Kikosi cha kocha Pep Guardiola pia kinauingia mwaka 2022 na rekodi ya kushinda mechi 10 mfululizo za Ligi Kuu ya England.
CHELSEA YACHOMOLEWA DAKIKA YA MWISHO DARAJANI
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brighton & Hove Albion usiku wa Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Chelsea ilitangulia kwa bao la Romelu Lukaku dakika ya 28, kabla ya Danny Welbeck kuisawazishia Brighton dakika ya 90 na ushei. Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 20, ikisogea nafasi ya pili ikiwa inaizidi pointi moja tu Liverpool ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi na timu hizo zitamenyana Jumapili katika mechi ya kuwania nafasi ya pili. Manchester City ndio inaongoza mbio za ubingwa kwa mbali, ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 20 pia.
SALAH AKOSA PENALTI, LIVERPOOL YAPIGWA 1-0
- Get link
- X
- Other Apps
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah jana alikosa penalti Liverpool ikichapwa bao 1-0 na wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power. Mkwaju wa penalti wa Salah ulipanguliwa na kipa Kasper Schmeichel dakika ya 15 na alipojaribu kuunganisha mpira uliorudi ukagonga mwamba. Bao pekee la Leicester City lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Everton, Ademola Lookman dakika ya 59 na kwa ushindi huo katika mchezo wa 18 wanafikisha pointi 25 katika nafasi ya tisa. Kwa upande wao Liverpool wanabaki na pointi zao 41 katika nafasi ya pili, sawa na Chelsea ya tatu, wote wakiwa nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya timu zote kucheza mechi 19.
KMC CHUPUCHUPU KUPIGWA NA RUVU CHAMAZI, 1-1
- Get link
- X
- Other Apps
BAO la dakika ya mwisho la Charles Ilamfya limeinusuru KMC kupoteza mechi nyumbani baada ya kutoa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ilamfya alifunga bao hilo dakika ya pili na ya mwisho ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo huo, kufuatia Ruvu Shooting kutangulia kwa bao la Ally Kombo dakika ya 22. Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 11 katika nafasi ya 12 na Ruvu Shooting sasa ina pointi 10 katika nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 11. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
SIMBA SC YAMTUPIA ‘MAFURUSHI’ YAKE HITIMANA
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA wa Tanzania, SIMBA SC wameachana na kocha wao, Mnyarwanda Thierry Hitimana baada ya miezi mitatu tu kazini. Hitimana alitambulishwa kama kocha Msaidizi Simba Septemba 11 na baada ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa kujiuzulu Oktoba 26, Mnyarwanda huyo akakaimu nafasi ya Kocha Mkuu. Lakini kufuatia kuletwa kocha mpya, Mspaniola Pablo Franco Martin Novemba 10, Hitimana anaonyeshwa mlango wa kutokea Msimbazi.
MTIBWA SUGAR YAILAZA COASTAL UNION 1-0 MKWAKWANI
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Bao pekee la Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Salum Kihimbwa kwa penalti dakika ya 27. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar imefikisha pointi 10 na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 11.
MSUVA APANGWA NA ZAMALEK NA TIMU MBILI ZA ANGOLA
- Get link
- X
- Other Apps
NYOTA wa Tanzania, Simon Happygod Msuva, timu yake, Wydad Athletic ya Morocco, maarufu Wydad Casablanca imepangwa Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Zamalek ya Misri, Petro Atletico na GD Sagrada Esperanca za Angola. Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri wamepangwa Kundi A pamoja na timu ya zamani ya kocha wao, Pitso Mosimane Mamelodi Sundowns ya nyumbani kwao, Afrika Kusini na Al Hilal na Al Merriekh, zote za Sudan. Kundi B linaundwa na Raja Athletic ya Morocco pia, Horoya ya Guinea, ES Setif ya Algeria na AmaZulu ya Afrika Kusini, wakati Kundi C kuna Esperance na Etoile du Sahel, zote za Tunisia, CR Belouizdad ya Algeria na Jwaneng Galaxy ya Botswana. Msuva mwenye umri wa miaka 26 sasa, aliibukia Azam Academy mwaka 2010, kabla ya kucheza Moro United 2011 hadi 2012 alipohamia Yanga ambayo aliichezea hadi mwaka 2017 aliponunuliwa na Difaâ El Jadida ya Morocco pia alikocheza hadi 2020 aliponunuliwa na Wydad. Hadi sasa, Msuva ameichezea timu ya taifa ya Tanzania ‘Taif
SIMBA YAPANGWA CHAMA, KISINDA KOMBE LA SHIRIKISHO
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamepangwa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na RS Berkane ya Morocco wanayochezea Mzambia, Clatous Chama na Mkongo, Tuisila Kisinda. Chama aliwika Simba kwa misimu mitatu tangu 2018, kabla ya kuuzwa RS Berkane Julai mwaka huu, wakati Kisinda alicheza kwa watani wao, Yanga msimu mmoja kabla ya kuuzwa pia mwanzoni mwa msimu huu. Timu nyingine katika Kundi D ni ASEC Mimosa ya Ivory Coast na US Gendarmerie ya Niger, wakati Kundi A kuna Pyramids ya Misri, CS Sfaxien ya Tunisia, Al Ahly Tripoli ya Libya na ZANACO ya Zambia. Kundi B kuna TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Otohi ya Kongo-Brazzaville, Cotton Sport ya Cameroon na Al Masry ya Misri na Kundi C zipo JS Soura ya Algeria anayaochezea mchezaji mwingine wa zamani wa Simba, Adam Salamba, Al Ittihad ya Libya, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na mshindi wa jumla kati ya JS Kabylie ya Algeria na Royal Leopard ya Eswatini. Royal Leopard iliilaza JS Kabylie 1-0 katik
MAFUNDI WANAPOKUTANA, HESHIMA HUCHUKUA NAFASI YAKE
- Get link
- X
- Other Apps
VIUNGO, Mganda Khalid Aucho (28) wa Yanga na Ramadhan Chombo ‘ Redondo’ wa Biashara United (34) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-1. Wawili hawa waliibuka pamoja mwaka 2009, Redondo akitokea Ashanti na akacheza pia Simba, Azam FC, Villa Squad, Mbeya City, Friends Rangers na African Lyon kabla ya kujiunga na Biashara mwaka 2019. Kwa upande wake Aucho aliibukia Manispaa ya Jinja, akacheza hadi Maji (Water), Simba za kwao, Uganda, Tusker, Gor Mahia za Kenya, Baroka FC ya Afrika Kusini, Red Star Belgrade, OFK Beograd za Serbia, East Bengal, Churchill Brothers za India na El Makkasa ya Misri kabla ya kutua Yanga Agosti mwaka huu.
CAVANI ATOKEA BENCHI KUINUSURU KIPIGO MAN UNITED
- Get link
- X
- Other Apps
MSHAMBULIAJI mkongwe wa Uruguay, Edison Cavani ametokea benchi usiku wa Jumatatu na kuifungia bao la kusawazisha Manchester United ikitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Newcastle United Uwanja wa St James' Park. Cavani alifunga bao hilo dakika ya 71 baada ya kuingia mwanzoni tu mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa England, Mason Greenwood. Newcastle ilitangulia kwa bao la mapema tu, dakika ya saba la kiungo Mfaransa, Allan Saint-Maximin. Mashetani Wekundu walikuwa kando la ligi kwa siku 16 kutokana na kukabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji waliokuwa na maambukizi ya virusi vya corona. Kwa sare hiyo, Man United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 17 ikiwa nafasi ya saba, wakati Newcastle ya kocha Muingereza, Eddie Howe imetimiza pointi ya 11 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
SIMBA QUEENS YASHINDA 8-0, YANGA PRINCES YADROO
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA watetezi, Simba Queens wameendelea kugawa maumivu kwa wapinzani katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya kuichapa Oysterbay Girls 8-0 jioni ya leo Uwanja wa Mo SIMBA Arena, Bunju, Dar es Salaam. Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Aisha Djafar matatu, Opa Clement na Aisha Mnunka kila mmoja mawili, wakati la nane Oysterbay Girls walijifunga. Watani wao, Yanga Princess wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Fountain Gate Princess Uwanja wa Fountain Gate, Dar es Salaam.
CHELSEA YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 VILLA PARK
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Chelsea imeonyesha kuimarika tena baada ya ushindi wa ugenini wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham. Reece James alianza kujifunga dakika ya 28 kuipatia Aston Villa bao la kwanza, kabla ya Chelsea kuzinduka kwa mabao ya Jorginho , mawili na yote kwa penalti dakika ya 34 na 90 na ushei na mtokea benchi, Romelu Lukaku dakika ya 56. Kwa ushindi huo, The Blues wanafikisha pointi 41 katika mchezo wa 19, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, wakizidiwa tu wastani wa mabao na Liverpool ambao pia wana mechi moja mkononi. Aston Villa ambayo ilicheza bila kocha wake, Steven Gerrard ambaye aliwekwa kando baada ya vipimo kuonyesha ameabukizwa virusi vya corona, inabaki na pointi zake 22 za mechi 18 katika nafasi ya 10.
YANGA YATOKA NYUMA TENA KUILAZA BIASHARA 2-1
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Yanga SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Biashara walitangulia kwa bao la Atupele Green Jackson dakika ya pili tu, kabla ya mshambuliaji Fiston Kalala Mayele kuisawazishia Yanga SC dakika ya 40 kwa bao zuri la til-tak akimalizia krosi ya Mkongo mwenzake, beki Djuma Shabani kutoka upande wa kulia. Kiungo mkongwe Mrundi, Said Ntibanzokiza akaifungia bao la ushindi Yanga dakika ya 79 kwa penalti baada ya beki Abdulmajid Mangaro kumsukuma winga Mkongo, Jeses Moloko Ducapel upande ule ule wa kulia. Yanga inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 10 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi. Biashara United yenyewe baada ya kipigo cha leo ambacho ni cha tatu mfululizo ikitoka kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar Morogoro na 1-0 na Coastal Union nyumbani, Musoma inabaki na pointi zake nane
ARSENAL YAWAPA ZAWADI YA 5-0 MASHABIKI WAKE
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Arsenal imewapa zawadi nzuri mashabiki wake jioni ya leo baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya wenyeji, Norwich City FC Uwanja wa Carrow Road mjini Norwich, Norfolk. Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Bukayo Saka mawili, dakika ya sita na 67, Kieran Tierney dakika ya 44, Alexandre Lacazette kwa penalti dakika ya 84 na Emile Smith Rowe dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 32, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa pointi sita na Chelsea, baada ya timu zote kucheza mechi 18, wakati Norwich inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi zake 10 za mechi 17 sasa.
MAN CITY YAICHAPA LEICESTER 6-3 ETIHAD
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Manchester City wameendelea kufurahia matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 6-3 dhidi ya wenyeji, Leicester City jioni ya leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya tano, Riyad Mahrez kwa penalti dakika ya 14, İlkay Gündoğan dakika ya 21, Raheem Sterling mawili, moja kwa penalti dakika ya 25 na lingine dakika ya 87 akimalizia pasi ya Rúben Dias na Aymeric Laporte dakika ya 69. Kwa upande wao, Leicester City mabao yao yamefungwa na James Maddison dakika ya 55, Ademola Lookman dakika ya 59 na Kelechi Iheanacho dakika ya 65 ambaye pia ndiye mpishi wa mabao mengine yote mawili. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 44 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 18, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 22 za mechi 16 katika nafasi ya tisa.
DTB YAENDELEZA MOTO CHAMPIONSHIP, YAILAZA GWAMBINA 5-3
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya DTB imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ijulikanayo kama Championship baada ya ushindi wa 5-3 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza. DTB inafikisha pointi 30 na kuendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi nne zaidi ya Ihefu SC inayofuatia, wakati Gwambina inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi zake nne baada ya kucheza mechi 12.
PRISONS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KAITABA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Tanzania Prisons imezinduka kwa ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Bao pekee la Tanzania Prisons ambayo mechi mbili zilizopita ilifungwa 2-1 na Yanga mjini Sumbawanga na 1-0 na Geita Gold mjini Geita, bao lake pekee katika mchezo wa leo limefungwa na Marco Mhilu dakika ya 78 akimalizia pasi ya Jeremiah Juma. Kwa ushindi huo katika mechi ya 11, Tanzania Prisons inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya 10, wakati Kagera Sugar iliyopoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani leo kufuatia kufungwa 2-0 na Mbeya Kwanza Desemba 22, inabaki na pointi zake tisa katika nafasi ya 13 sasa kufuatia kucheza mechi 10.
YANGA SC YAITISHA MKUTANO WA MATAWI JUMATATU JANGWANI
- Get link
- X
- Other Apps
MKONGWE WA KONGO DEO KANDA ATUA MTIBWA SUGAR
- Get link
- X
- Other Apps
KLABU ya Mtibwa Sugar imemtambulisha winga mkongwe wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Deo Kanda A Mukok kuwa mchezaji wake mpya wa kwanza katika dirisha hili dogo la Usajili. Kanda pamoja na kuwika AS Vita ya Kinshasa na TP Mazembe, DC Motema Pembe za Lubumbashi, kwao DRC na Raja Casablanca ya Morocco, pia amewahi kucheza Simba SC ya Dar es Salaam.
RASMI, SURE BOY NI MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC
- Get link
- X
- Other Apps
KIUNGO Salum Abubakar 'Sure Boy' ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa kwanza wa Yanga SC katika dirisha dogo la usajili. Sure Boy anajiunga na Yanga, timu ambayo baba yake aliichezea kati ya mwaka 1986 na 1993 baada ya kuachana na Azam FC aliyojiunga nayo mwaka 2007. Sure Boy ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuishukuru Azam FC kwa kumkuza kisoka. "Assalam Alaykum, Nitumie Fursa Hii Kushukuru Management, Technical Staff, Makocha, Viongozi, Mashabiki, Wachezaji Wenzangu Na Wafanyakazi Wote Wa @azamfcofficial Tuliofanya Kazi Kwa Pamoja Kwa Ushirikiano Kwa Kipindi Kirefu Sana. Nyakati Za Huzuni, Majonzi Na Furaha Zote Tulisimama Pamoja Kuipigania Team Kwa Jasho Na Damu. Nimeishi Kama MwanaFamilia Kwa Miaka Yote Hapo Klabuni, Nilikuja Nikiwa Kijana Mdogo Sana . Naondoka Kutafuta Changamoto Mpya Nikiwa Nimepuvuka Kimwili Na Kiakili. Mimi Ni Binaadamu Kama Kuna Sehemu Nimewakosea Naombeni Mnisamehe Na Mimi Pia Nimesamehe Kama Mlinikosea. Asanteni Sana @aza
YANGA PRINCESS WASHINDA 2-0 DOM LIGI YA WANAWAKE
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Yanga Princes imeanza vyema Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Bao Bab Queens Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mabao yote ya Yanga Princes leo yamefungwa na mshambuliaji chipukizi wa kimafaifa wa Tanzania, Aisha Masaka yote kipindi cha pili. Mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Wanawake leo, JKT Queens imeichapa Oysterbay Girls 3-1 Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Mbweni, The Tigers Queens wameichapa TSC Queens 4-0 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Fountain Gate Princess wameshinda 4-0 dhidi ya Ilala Queens Uwanja wa Fountain Gate, Dar es Salaam. Ikumbukwe jana mabingwa watetezi, Simba Queens, walishindi wa 15-0 dhidi ya Ruvuma Queens Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam, mabao yake yakifungwa na Zena Khamis matatu, Asha Djafar matatu, Opa Clement matatu, Jacqueline Albert matatu, Aisha Juma na mawili Ruvuma Queens walijifunga. Mechi nyingine ya jana, wenyeji, Alliance Girls walishindi wa 1-0 dhidi ya Mlandizi Q