AISHA MASAKA APIGA HAT-TRICK YANGA PRINCESS YASHIDA 3-1


TIMU ya Yanga Princess imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya JKT Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao yote ya Yanga Princess leo yamefungwa na mshambuliaji nyota na chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Aisha Masaka ‘Aisha Magoal’ dakika za 35,38 na 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Yanga Princess inapanda kileleni japo kwa muda, ikifikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Simba Queens ambao hata hivyo wamecheza mechi mbili.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA