Posts
Showing posts from February, 2022
LIVERPOOL WATWAA CARABAO KWA MATUTA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 11-10 kufuatia sare ya 0-0 na Chelsea usiku huu Uwanja wa Wembley Jijini London. Kipa Kepa Arrizabalaga aliyeingia dakika ya 119 maalum kwenda kuokoa mikwaju ya penalti, hakuweza kuokoa hata moja na bahati mbaya zaidi kwake akaenda kupiga juu ya lango penalti yake ya mwisho. Waliofunga penalti za Liverpool ni Jamaa Milner, Fabinho, Virgil van Dijk, Trent Alexander-Arnold, Mohamed Salah, Diogo Jota, Divock Origi, Andrew Robertson, Harvey Elliott, Ibrahima Konaté na kipa Caoimhin Kelleher. Waliofunga penalti za Chelsea ni Marcos Alonso, Romelu Lukaku, Kai Havertz, Jorginho, Antonio Rüdiger, N'Golo Kanté, Timo Werner, Thiago Silva na Trevoh Chalobah.
MAYELE ATETEMA MARA MBILI, YANGA YAITANDIKA KAGERA 3-0
- Get link
- X
- Other Apps
VINARA, Yanga SC wameuanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kagera Sugar usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele mawili dakika ya 30 na 50 na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 64. Yanga ingeweza kuondoka na ushindi mnoni zaidi kama si wachezaji wake, Mayele, Ntibanzokiza na mtokea benchi, mshambuliaji Mkongo mwingine, Heritier Makambo kupoteza nafasi nzuri za kufunga. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 16 na kutanua uongozi wake kwa pointi 11 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi. Kagera Sugar baada ya kupoteza mechi ya leo, wanabaki na pointi zao 20 za mechi 16 sasa katika nafasi ya nane.
MBEYA CITY YAICHOMOLEA PRISONS JIONI KABISA, 1-1
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU za Tanzania Prisons na Mbeya City zimegawana pointi baada ya sare ya 1-1 jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Adili Buha alianza kuifungia Prisons dakika ya saba, kabla ya Ssemuju Joseph kuisawazishia Mbeya City dakika ya 86. Kwa sare hiyo, Mbeya City inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC ambayo pia ina mechi moja mkononi. Hali ni mbaya kwa Tanzania Prisons ambayo baada ya sare ya leo inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuzibeba timu nyingine 15 kwenye Ligi Kuu. Mechi iliyotangulia mchana wa leo, wenyeji, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 pia na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Waziri Junior alianza kuifungia Dodoma Jiji dakika ya 11, kabla ya Abrahman Mussa kuisawazishia Ruvu Shooting dakika ya 58. Ruvu Shooting inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 16 na kurejea nafasi ya 12, wakati Dodoma Jiji
MAMEMLODI YAICHAPA AHLY 1-0 CAIRO
- Get link
- X
- Other Apps
BAO pekee la kiungo Thapelo James Morena dakika ya 85 jana liliwapa Mamelodi Sundowns ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Misri. # MSIMAMO KUNDI A MP W D L F A D P Last 5 matches H2H 1 Mamelodi Sundowns 3 2 1 0 2 0 +2 7 W D W 2 Al Merreikh 2 1 1 0 2 1 +1 4 W D 3 Al Ahly 2 0 1 1 0 1 -1 1 L D 4 Al Hilal Omdurman 3 0 1 2 1 3 -2 1 L D L MATOKEO - CAF Champions League jana FT ES Tunis 0 - 0 Etoile du Sahel View events FT Galaxy 1 - 2 Belouizdad View events FT Sagrada Esperança 0 - 1 Petro de Luanda View events FT Al Ahly 0 - 1 Mamelodi Sundowns View events FT Wydad Casablanca 3 - 1 Zamalek
ABRAMOVICH AJIWEKA KANDO UENDESHAJI CHELSEA
- Get link
- X
- Other Apps
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich amekabidhi usimamizi na uendeshaji wa klabu yake hiyo kwa taasisi ya hisani, kuonyesha amekataa wito wa kumtaka aachie ngazi kufuatia nchi yake, Urusi kuivamia Ukraine. Bilionea huyo ambaye amekuwa mmiliki wa Chelsea tangu mwaka 2003, hajatoa tamko lolote juu ya vita huyo. Abramovich amewekeza kiasi cha zaidi ya dola za Kimarekani Bilioni 2 Chelsea, na kuifanya klabu hiyo na mafanikio Zaidi England. Tangu Abramovich aichukue Chelsea imeshinda mataji 19 jumla na ndio mabingwa wa sasa Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
MAN CITY YAICHAPA EVERTON 1-0 GOODISON PARK
- Get link
- X
- Other Apps
BAO pekee la kiungo Philip Foden dakika ya82 jana limeipa Manchester City FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Everton FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park, Liverpool. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 66 katika mchezo wa 27 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi sita zaidi ya Liverpool, ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi, wakati Everton inabaki na pointi zake 22 za mechi 24 nafasi ya 17.
MAN UNITED YAAMBULIA POINTI MOJA KWA WATFORD
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford. Man United inafikisha pointi 47 baada ya sare hiyo katika mchezo wa 27, ikiendelea kushika nafasi ya nne kwa pointi mbili zaidi ya Arsenal ambayo hata hivyo ina mechi tatu mkononi. Kwa upande wao, Watford wanafikisha pointi 19, ingawa inabaki nafasi ya 19, ikiizidi pointi mbili tu Norwich City inayoshika mkia baada ya timu zote kucheza mechi 26.
KMC YAIMIMINIA POLISI TZ 3-1 CHAMAZI
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, KMC imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya KMC yamefungwa na Iddi Kipagwile dakika ya 15, Emmanuel Mvuyekure dakika ya 73 na Sadallah Lipangile dakika ya 88. Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 22 katika nafasi ya sita, wakati Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 19 katika nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 16.
MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-1 SOKOINE
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Mayanja Mululi dakika ya 38 na Omary Sultan dakika ya 75, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Habib Kyombo kwa penalti dakika ya 41. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 13, ikishukia nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
GEITA, NAMUNGO ZAFUNGUA MZUNGUKO WA PILI KWA SARE
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa kwanza kabisa wa duru la pili Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Geita Gold walitangulia kwa bao la George Mpole dakika ya 73, hilo likiwa bao lake la nane la msimu, kabla ya Iddi Farjala kuisawazishia Namungo FC dakika ya 84. Kwa sare hiyo, Namungo FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 16, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Azam FC zikifuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Geita Gold inafikisha pointi 21 mechi 16 nafasi ya sita.
GABASKI AKUTANA NA MAKIPA WA SIMBA CASABLANCA
- Get link
- X
- Other Apps
KIPA wa Zamalek ya Misri, Mohamed Qotb Abou Gabal Ali, ‘Gabaski’ akiwa na makipa wa Simba SC, Aishi Manula, Abdul Salum na Beno Kakolanya Jijini Casablanca nchini Morocco jana. Wakati Zamalek itamenyana na wenyeji, Wydad Athletic kesho katika mechi ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba watamenyana na wenyeji wengine, RSB Berkane Jumapili katika mechi ya Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika. Gabaski aling’ara kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika akiisaidia Misri kufika fainali kabla ya kufungwa na Senegal kwa penalti nchini Cameroon.
ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-0 EMIRATES
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London. Hwang Hee-chan aliifungia Wolves bao la kuongoza dakika ya 10, kabla ya Arsenal kutoka nyuma kwa mabao ya Nicolas Pepe dakika ya 82 na Alexandre Lacazette aliyemlazimisha Jose Sa kujifunga dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 45 katika mchezo wa 24 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Manchester United ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi, wakati Wolves inabaki na pointi zake 40 za mechi 25 nafasi ya saba.
LIVERPOOL YAISHINDILIA LEEDS 6-0 ANFIELD
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield usiku wa Jumatano. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohammed Salah kwa penalti yote mawili, dakika ya 15 na 35, Joel Matip dakika ya 30, Sadio Mane mawili pia dakika ya 80 na 90 na beki Virgil Van Dijk dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 60, sasa ikizidiwa tatu tu na Mabingwa watetezi, Manchester City baada ya timu zote kucheza mechi 26, wakati Leeds inabaki na pointi zake 23 za mechi 25 nafasi ya 15.
MAN U YAPATA SARE MADRID NA ATLÉTICO
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Atletico Madrid wamelazimishwa sare ya 1-1 na Manchester United katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja we Wanda Metropolitano Jijini Madrid. Joao Felix alianza kuwafungia wenyeji, Atlético dakika ya saba, kabla ya Anthony Elanga kuisawazishia Manchester United dakika ya 80.
YANGA SC YAWAPIGA MTIBWA 2-0 MANUNGU
- Get link
- X
- Other Apps
VIGOGO, Yanga SC wamekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzonkiza dakika ya 45 na ushei na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 66. Kwa ushindi huo, Yanga inakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi na pointi 39, nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wamecheza mechi 15. Mtibwa Sugar baada ya kipigo cha kwanza nyumbani, Manungu msimu huu wanabaki na pointi zao 12 za mechi 15 nafasi ya 15 Ligi ya timu 16, ambayo mwishowe mbili zitateremka moja kwa moja na mbili kwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.
CHELSEA YAICHAPA LILLE 2-0 LONDON
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Kai Havertz dakika ya nane na Christian Pulisic dakika ya 63 na kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi watahitaji sare ugenini ili kwenda Robo Fainali.
BIASHARA UNITED YAICHAPA AZAM FC 2-0 KIRUMBA
- Get link
- X
- Other Apps
MABAO ya Collins Opare dakika ya 49 na James Shagara dakika ya 90 na ushei yameipa Biashara United ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Kwa ushindi huo, Biashara inafikisha pointi 15 na kumaliza mechi 15 za mzunguko wa kwanza katika nafasi ya 12, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 24 za mechi 15 pia katika nafasi ya tatu.
NAMUNGO FC YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 ILULU
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Namungo FC jana wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Ilulu mjini Lindi. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya 40 na Relliant Lusajo dakika ya 48 na kwa huo wanafikisha pointi 23 na kumaliza mechi ya 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu katika nafasi ya nne, wakiziwa moja tu na Azam FC inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na mechi moja mkononi pia. Mbeya City inabaki na pointi zake 23 za mechi 15 pia nafasi ya tano.
SIMBA NA PAMBA, YANGA NA GEITA NUSU FAINALI ASFC
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA watetezi, Simba SC watamenyana na Pamba FC ya Mwanza katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup ( ASFC), wakati watani wao, Yanga watamenyana na Geita Gold. Mechi nyingine za Robo Fainali ni Azam FC na Polisi Tanzania na Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar. Mshindi kati ya Simba SC na Pamba FC atamenyana na mshindi kati ya Yanga na Geita Gold katika Nusu Fainali na mshindi kati ya Azam FC na Polisi Tanzania atakutana na mshindi kati ya Coastal Union na Kagera Sugar.
TOTTENHAM YAILAZA MAN CITY 2-1 ETIHAD
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA watetezi, Manchester City wamechezea kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Tottenham Hotspur jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad. Mabao ya Spurs jana yamefungwa mshambuliaji wa kimataifa wa England, Harry Kane aliyefunga mabao mawili dakika ya 59 na 90 na ushei Riyad Mahrez kwa penalri dakika ya 90 na ushei na wakati ya Man City yamefungwa na 4' Dejan Kulusevski1 dakika ya nne na 59 na First nam İlkay Gündoğan dakika ya 33. Tottenham Hotspur inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya saba, wakati Man City inaendelea kuongoza ligi kwa pointi zake 63 za mechi 26.
ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 2-1 EMIRATES
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Emirates Jijini London. Arsenal inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 23, ingawa inabaki nafasi ya sita, wakati Brentford inabaki na pointi zake 24 za mechi 26 katika nafasi ya 14. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 48 na Bukayo Saka dakika ya 79, wakati la Brentford limefungwa na Christian Norgaard dakika ya 90 na ushei.
LIVERPOOL YAICHAPA NORWICH CITY 3-1 ANFIELD
- Get link
- X
- Other Apps
WENYJI, Liverpool jana waliitandika Norwich City mabao 3-1 Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Milot Rashica alianza kuifungia Norwich dakika ya 48, kabla ya Liverpool kutoka nyuma kwa mabao ya Sadio Mané dakika ya 64, Mohamed Salah 67 na mchezaji mpya, Luis Díaz 81. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 25, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi sita na vinara, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi.
GEITA GOLD YAICHAPA COASTAL 2-0, POLISI 0-0 KAGERA
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Mabao ya Geita Gold yamefungwa na George Mpole kwa penalti dakika ya 38 na Danny Lyanga dakika ya 41 na kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 15 na kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi katika nafasi ya nne. Coastal Union, mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 1988, wanakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi wakiwa na pointi 17 katika nafasi ya tisa. Mechi nyingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Kagera Sugar inafikisha pointi 20 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya saba, wakati Polisi inafikisha pointi 19 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi.
SIMBA SC SAFARI NIGER KWA MAJUKUMU YA KIMATAIFA
- Get link
- X
- Other Apps
MASAFARA wa Simba umefika salama Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambako wachezaji watalala kabla ya kuunganisha ndege kesho asubuhi kwenda nchini Niger. Ikumbukwe Jumapili Simba watakuwa na mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, US Gendarmerie kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Simba Sports Jénérali Seyni Kountché Jijini Niamey.
REFA KOMBA KUCHEZESHA AMAZULU NA SETIF AFRIKA KUSINI
- Get link
- X
- Other Apps
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua refa wa Tanzania, Frank Komba kuwa miongoni mwa Waamuzi watakaochezesha mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Amazulu na ES Sètif ya Algeria) Februari 25, mwaka huu Uwanja wa Mosses Mabhida, Durban nchini Afrika Kusini. Aidha, CAF pia imewateua marefa wa kike wa Tanzania, Florentina Zablon, Janeth Balama, Glory Tesha na Tatu Malogo kuchezesha mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia kwa Wanawake U20 baina ya Ethiopia na Ghana Machi 13, mwaka huu Uwanja wa Abebe Bekila, Jijini Addis Ababa, Ethiopia. CAF pia imemteua Meneja wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB), Jonathan Kasano kuwa Mratibu wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya ndugu, Al Merrikh na Al Hilal Februari 25, mwaka huu Jijini Khartoum nchini Sudan. Naye Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto ameteuliwa na CAF kuwa Mratibu wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya ndugu pia, GD Sagrada Esperança na Petro Atlético Februar
YANGA YAGAWA KADI ZA KIELEKTRONIKI BUNGENI
- Get link
- X
- Other Apps
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akikabidhi kadi ya Uanachama ya Kielektroniki kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Kapteni Mstaafu, George Huruma Mkuchika na Waheshimiwa Wabunge katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya za uanachama za Yanga leo Bungeni Jijini Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akikabidhi kadi ya Uanachama ya Kielektroniki kwa Wabunge katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya za uanachama za Yanga leo Dodoma.