AZIZ KI NI MCHEZAJI MPYA NA HALALI WA YANGA SC
KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji wake mpya wa kuelekea msimu ujao.
Aziz Ki anakuwa mchezaji mpya wa tano Yanga SC baada ya beki Mkongo, Lomalisa Mutambala kutoka Sagrada Esperança ya Angola, kiungo Mrundi, Gael Bigiriamana kutoka Glentoran ya Ireland Kaskazini, winga Mghana, Bernard Morrison kutoka Simba na mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Comments
Post a Comment