MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YASHINDA 5-1 KIGAMBONI


MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 5-1 katika mchezo wa Kirafiki dhidi ya Transit Camp Ijumaa Uwanja wa Avic Town, Somangira nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na washambuliaji wake Wakongo, Fiston Kalala Mayele matatu, Heritier Makambo na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki moja kila mmoja.


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YAAFIKI KUCHEZA ZANZIBAR MARUDIANO NA BERKANE