TIMU ya Yanga imefanikiwa kutwaa Kombe la Muungano, michuano maalum ya kuazimisha sherehe za miaka 61 ya Muungano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU usiku huu Uwanja wa Gombani, Pemba. Shujaa wa Yanga leo ni kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Maxi Mpia Nzengeli aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45 na mabingwa hao wa Tanzania Bara wamezawadiwa Sh. Milioni. Pamoja na kufunga bao la ushindi, Nzengeli pia ameshinda Tuzo za Mfungaji Bora kwa mabao yake mawili jumla na Nyota wa Mchezo wa leo, wakati kiungo mwenzake wa Yanga, Mudathir Yahya Abbas ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano. JKU, mabingwa wa Zanzibar kwa kumaliza nafasi ya pili wamezawadiwa Sh. Milioni 30. Jumla ya timu nane zimeshiriki michuano ya mwaka huu iliyoanzia hatua ya Robo Fainali, nyingine ni KMKM, Zimamoto na KVZ, zote za Zanzibar na Azam FC, Coastal Union na Singida Black Stars za Tanzania Bara. Mabingwa wa msimu uliopita, Simba hawakushiriki mic...
Comments
Post a Comment