KLABU 13 zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST yaliyopangwa kufanyika Februari 25 na 26 kwenye Bwawa la Kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki. Meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe amezitaja klabu hizo kuwa Dar es Salaam Swim Club (DSC), Bluefin, Morogoro Piranhas, Mwanza Swim Club, Wahoo Zanzibar, FK Blue Marlins na klabu kutoka Uganda Flash Swim Club. Klabu nyingine ni Braeburn Arusha, Premiere Swim Club (Dar es Salaam), Mwanza Swim Club, Lake Swim Club, Taliss-IST na HPT. Muogeleaji Lina Goyayi akichapa maji katika mashindano yaliyopita Hadija alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na waogeleaji wanafanya mazoezi ili kushindania zawadi mbalimbali siku hiyo. Alisema kuwa waogeleaji zaidi ya 200 wanatarajia kushiriki katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na International School of Tanganyika (IST), Bwana Sukari, Pepsi, Jubilee Insurance, Dehli Darbaar, Wrap and Roll, F and L Juices na Burgers 53. K