HAALAND APIGA TANO MAN CITY YAITANDIKA LEIPZIG 7-0


WENYEJI, Manchester City wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa kishindo wa mabao 7-0 dhidi ya Red Bull Leipzig usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Erling Haaland matano akiiadhibu timu ya Bundesliga dakika za 22 kwa penalti, 24, 45 na ushei, 53 na 57, Nahodha Ilkay Gundogan dakika ya 49 na Kevin De Bruyne dakika ya 90 na ushei.
Kwa matokeo hayo, Manchester City iliyo chini ya kocha Mspaniola, Pep Guardiola inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 8-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Ujerumani.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA