Posts

Showing posts from May, 2023

KIKOSI CHA YANGA KIMACHOKWENDA ALGERIA KUWAVAA TENA USM ALGER

Image
HII ndio orodha ya wachezaji wa Yanga wanaoomdoka leo kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili Jijini Algiers.  Yanga inahitaji ushindi wa 2-0 ili kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kutwaa Kombe la Afrika baada ya kufungwa 2-1 kwenye mechi ya kwanza Dar es Salaam Jumapili iliyopita.

TANZANIA KUCHEZA NA KONGO KUFUZU OILIMPIKI YA WANAWAKE PARIS 2024

Image
TANZANIA itaanza na Kongo katika Raundi ya Kwanz aya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Michezo ya Olimpiki (WOFT) Paris 2024 nchini Ufaransa. Ikifanikiwa kuitoa Kongo, Tanzania itakutana na mshindi kati ya Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Jumla ya timu 25 zimeingia kwenye mchujo wa kuwania tiketi ya Olimpiki mwakani, huku 18 zikienda moja kwa moja Raundi ya Kwanza na saba zilizobaki zikiongozwa na mabingwa, Afrika Kusini ambazozipo nafasi za juu kwenye renki baada ya Fainali za Kombe la Mataifa ya afrika mwaka jana (WAFCON) zitaanzia Raundi ya Pili. Washindi tisa wa Raundi ya Kwanza zitaungana na saba za renki za juu kwa ajili ya Raundi ya Pili itakayohusisha timu 16 na washindi nane watasonga Raundi ya Tatu, kisha nne zitamenyana katika Raundi ya Nne. Washindi wawili wa Raundi ya Nne watafuzu kwenye Fainakli ya Michezo ya ya Paris mwakani. Kwenye Olimpiki ya mwaka jana Jijini Tokyo nchini Japan, Zambia iliiwakilisha Afrika, na sasa She-polopolo

MWAMEJA AKUMBUSHIA SAFARI YA SIMBA FAINALI CAF 1993

Image
 

MTANZANIA KUWA KAMISHNA FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Mtanzania, Ahmed Mgoyi kuwa Kamishna wa mchezo wa Fainali ya Ligi ya kwanza ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Al Ahly dhidi ya Wydad AC Morocco Juni 4 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri. Ahmed maarufu kama Msafiri Mgoyi ni Mjumbe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kigoma (KRFA) na mmoja katĂ­ ya viongozi wasoefu wa Soka nchini.

RAIS WA TFF KARIA ATOA POLE JANGA LA JANA MKAPA

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametoa kwa pole kwa shabiki mmoja aliyefariki dunia jana wakati wa mchezo wa Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga na USM Alger Uwanja wa BenjamĂ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI AWAKABIDHI YANGA MILIONI 20 ZA RAIS DK SAMIA

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Pindi Chana (kushoto) akimkabidhi kipa wa Yanga, Metacha Mnata fedha taslimu Sh. Milioni 20 zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa bao lao wakifungwa 2-1 na USM Alger Jumapili kwenye Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa BenjamĂ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam.

SIMBA YATOA POLE KIFO CHA SHABIKI YANGA NA USM ALGER

Image
KLABU ya Simba imetoa pole kwa kifo cha shabiki mmoja na wengine 30 waliojeruhiwa wakati wa mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika katĂ­ ya Yanga USM Alger ya Algeria Jumapili Uwanja wa BenjamĂ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam.

MMOJA AFARIKI, 30 WAJERUHIWA YANGA NA USM ALGER DAR

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewajulia hali majeruhi 10 wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke waliojeruhiwa kutokana na tukio la kukanyagana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wakijiandaa kuingia kutazama mechi kati ya Yanga na USM Alger ya nchini Algeria katika mchezo wa Kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliocheza Mei 28, 2023. Chana alipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Joseph Gasper Kimaro kwamba, walipokea majeruhi 30 ambapo wanaume walikua 18, Wanawake 10 na mtoto Mmoja ambapo mgonjwa mmoja alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu. Ameeleza kuwa mpaka sasa wamebakiwa na wagonjwa 10 na wote wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika. Chana katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwana

MAN UNITED YAICHAPA FULHAM 2-1 DE GEA AOKOA PENALTI

Image
TIMU ya Manchester United imehitimisha msimu wa Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Jadon Sancho dakika ya 39 na Bruno Fernandes dakika ya 55 baada ya Fulham kutangulia na bao la Kenny Tete dakika ya 19, huku kipa David de Gea akiokoa mkwaju wa penalti wa Aleksandar Mitrovic dakika ya 26. Kwa ushindi huo, Manchester United inamaliza na pointi 75 nafasi ya tatu na Fulham inamaliza na pointi 52 nafasi ya 10.

XHAKA APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA WOLVES 5-0

Image
KOCHA Mikel Arteta amemalizia vizuri Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya  Wolverhampton Wanderers leo Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Granit Xhaka mawili dakika ya 11 na 14, Bukayo Saka dakika ya 27, Gabriel Jesus dakika ya 58 na Jakub Kiwior dakika ya 78. Kwa ushindi huo, Arsenal inamaliza Ligi na pointi 84, nyuma ya mabingwa Manchester City wenye pointi nne zaidi, wakati Wolves wanamaliza na pointi 41 nafasi ya 13.

AISHI MANULA KWENDA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Image
KIPA namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu baada ya tiba zake kugonga mwamba nchini. Aishi aliumia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Aprili 7, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

YANGA YAJIWEKA PAGUMU FAINALI SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-1 NYUMBANI

Image
TIMU ya Yanga imeshindwa kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, BenjamĂ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam baada ya kufungwa mabao 2-1 na USM Alger katika mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mabao ya USM Alger yamefungwa na mshambuliaji Aimen Mahious dakika ya 32 na kiungo Islam Merili dakika ya 84, wakati la Yanga limefungwa na mshambuliaji wake Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 82. Sasa Yanga wanakabiliwa na mtihani mgumu we kwenda kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers Jumapili ijayo.

RAIS YANGA SC AITISHA MKUTANO MKUU WA MWAKA SAA CHACHE

Image
RAIS wa Yanga SC, Hersi Ally Said ameitisha Mkutano Mkuu wa mwaka utakaofanyika Juni 24, mwaka huu Jijini Dar es Salaam. Tangazo la Mkutano huo linakuja Saa chache kabla ya mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ikimemyana na USM Alger leo Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

KACHUMBARI ALIYEWIKA SMALL SIMBA, MLANDEGE NA MALINDI AFARIKI DUNIA

Image
ALIYEWAHI kuwa beki wa timu za Kikwajuni, Small Simba, Mlandege, Malindi SC na Mafunzo, zote za Zanzibar, Mohamed Kachumbari (pichani kushoto) amefariki dunia asubuhi ya leo Jijini Dar es Salam. Taarifa za watu wa karibu wa marehemu zimesema, mwili wake umesafirishwa mchana wa leo kutoka Dar kwenda nyumbani kwao, Mwanakwerekwe Zanzibar kwa mazishi. Pamoja na Kikwajuni, Small Simba, Mlandege, Malindi SC na Mafunzo, marehemu Kachumbari pia alichezra timu ya taifa ya Zanzibar, 'Zanzibar Heroes' na ya Tanzania, 'Taifa Stars'. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin. Mohamed Kachumbari, wa tatu kutoka kuliawaliosimama akiwa na kikosi cha Small Simba ya Zanzibar mwaka 1991 Jijini Mbabane, Swaziland (sasa Ewatini) kabla ya mechi ya marudiano Raundi ya Awali Kombe la Washindi Afrika dhidi ya wenyeji, Highlanders.  Wengine kulia ni Meneja, Hussein Lee na kipa Ridhaa Hamisi. Kushoto kwa Kachumbari ni Duwa Said, Karume Mussa, Ubwa Makame 'Mzungu', Innocent Haule, Rashi

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA TAYARI UMEFURIKA YANGA V USM ALGER

Image
TIKETI zote 60,000 za madaraja tofauti ya mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Yanga na USM Alger ya Algeria kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam zimeuzwa. Maana yake Uwanja umekwishasheheni Saa 30 na ushei kabla ya mchezo wenyewe, ambao utafuatiwa mechi ya marudiano Juni 3 Jijini Algiers Julai 5, 1962 Jijini Algiers. Mechi hiyo itachezeshwa na refa, Jean-Jacques Ngambo Ndala atakayesaidiwa na Olivier Kabene Safar wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini watakaokuwa wanakimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja kulia na kushoto. Kufika hatua hii, Yanga iliitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati USM Alger iliitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.

MAZOEZI YA YANGA JANA KIGAMBONI KUIKABILI USM ALGER KESHO

Image
KIPA wa Yanga raia wa Mali, Djigui Diarra akitoa maelekezo kwa wenzake wakati wa mazoezi ya jana Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Yanga inajiandaa na mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Juni 3 Jijini Algiers. PICHA: MAZOEZI YA YANGA SC JANA AVIC TOWN

BILIONEA GHALIB AAHIDI MILIONI 63 KILA MCHEZAJI YANGA

Image
MFADHILI Mkuu wa Yanga SC, Ghalib Said Mohamed ameahidi zawadi ya Sh. Milioni 63 kwa kila mchezaji iwapo watatwaa Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga watawakaribisha USM Alger ya katika mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo zitarudiana Juni 3 Jijini Algiers nchini Algeria.

DUBE NA MAYELE KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA ASFC

Image
WACHEZAJI wawili wa Azam FC, Prince Dube Mpumelelo na Abdul Suleiman Sopu watachuana na wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, Clement Mzize na Fiston Kalala Mayele kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

MAN UNITED YAICHAPA CHELSEA 4-1 NA KUFUZU LIGI YA MABINGWA

Image
TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Chelsea kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Carlos Casemiro dakika ya sita, Anthony Martial dakika ya 45 na ushei, Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 73 na Marcus Rashford dakika ya 78, wakati la Chelsea limefungwa na JoĂŁo FĂ©lix dakika ya 89. Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 72 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 37. Ni matokeo ambayo yanaihakikishia Manchester United kurejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ambao ni mwanzo mzuri kwa kocha Mholanzi, Erik ten Hag kwenye msimu wake wa kwanza. Kwa upande wao Chelsea kipigo hicho kinawaacha na pointi zile zile 43 za mechi 37 pia nafasi ya 12.

SIMBA SC YAAJIRI MTAALAMU WA KUSAKA VIPAJI

Image
KLABU ya Simba SC imemtambulisha Mholanzi, Mels Daalder kuwa Mkuu wake wa Idara ya kusaka vipaji vya kusajili kwneye timu yake kuelekea msimu ujao. Daalder amebeba matumaini makubwa ya uongozi wa Simba kutokana na uzoefu wake wa kufanya na kazi na klabu kubwa ikiwemo Manchester United.

YANGA YAANZA KUMKABILI FEI TOTO KWA UTOVU WA NIDHAMU

Image
KLABU ya Yanga imemtaka kiungo wake, Feisal Salum Abdallah kufika mbele ya Kamati yake ya Sheria na Nidhamu kujibu tuhuma za utovu wa Nidhamu zinazomkabili.

MAN CITY YAAMBUA SARE KWA BRIGHTON THE AMEX

Image
MABINGWA mara tatu mfululizo, Manchester City usiku wa jana wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa The AMEX, Falmer, East Sussex. Phil Foden alianza kuifungia Manchester City dakika ya 25, kabla ya Julio Enciso kuisawazishia Brighton & Hove Albion dakika ya 38. Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi 89 pale juu sasa ikiizidi pointi nane Arsenal baada ya wote kucheza mechi 37, wakati Brighton imefikisha pointi 62 za mechi 37 pia nafasi ya sita.

MKUU MPYA WA MKOA DAR ANUNUA TIKETI 1,000 YANGA NA USM ALGER

Image
MKUU mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamilla amenunua tiketi za Sh. Milioni 5 kwa ajili ya mashabiki kuelekea mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC dhidi ya USM Alger Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Chalamila amemkabidhi Fedha hizo Rais wa Yanga, Hersi Said ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam na akasema atakabidhiwa mwenyewe tiketi hizo 1,000 akazigawe kwa watu wa kipato cha chini wakaishangilia Yanga Jumapili. Pamoja na fedha hizo, Chalamila amekabidhi Sh. Milioni 5 nyingine kwa ajili ya kutayarishwa chakula cha jioni baada ya mchezo huo ili pamoja na wachezaji siku hiyo. Naye Rais wa Yanga SC, Hersi Said alimkabidhi RC Chalamila jezi ya kijani ya timu hiyo aivae siku ya Jumapili. Mchezo huo utachezeshwa na refa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngambo Ndala atakayesaidiwa na Mkongo mwenzake, Olivier Kabene Safar na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini wat

BENKI YA NBC YAZINDUA MBIO ZA NBC DODOMA MARATHON 2023

Image
• Mbio za NBC Dodoma Marathon kufanyika tarehe 23.07.2023  Dodoma • Itahusisha mbio za Km42, Km21, Km10 na Km5 • Mbio zinalenga kukusanya fedha kusaidia kuboresha afya ya mama na mtoto. • Zaidi ya wakimbiaji 6,000 kutoka nchi mbalimbali kushiriki • Ili kujisajiri tembelea  www.events.nbc.co.tz  na kuchangia kiasi cha TZS 30,000 kwa usajili au 25,000 kwa kundi la kuanzia watu ishirini. • Zaidi ya shilingi 500 milioni zimekusanywa katika miaka mitatu iliyopita, zikigharamia matibabu ya saratani kwa zaidi ya wanawake 1,300 • Benki kuanza kutoa udhamini kwa wanafunzi wanosomea ukunga ili kusaidia upungufu wa wataalamu hao nchini. Dar es Salaam, 23 Mei 2023. Benki ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC Dodoma Marathon mwaka 2023 siku ya Jumapili tarehe 23 Julai 2023 mkoani wa Dodoma. Lengo kuu la mbio za NBC Dodoma Marathon ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kuchangia kutoa ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wanaosomea taal

NYOTA WA POLISI TANZANIA TISHIO KWA MABAO YA VICHWA LIGI KUU

Image
MSHAMBULIAJI wa Polisi Tanzania, Kelvin Kongwe Sabato ‘Kiduku’ wa Polisi Tanzania ndiye anaongoza kwa kufunga mabao ya kichwa katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inayoelekea ukingoni.

MABAO 12 MAYELE AMEFUNGA KWA GUU LA KULIA LIGI KUU YA NBC

Image
MSHAMBULIAJI Mkongo wa Yanga SC, Fiston Kalala Mayele katika mabao 16 yanayomuweka kileleni kwenye chati ya ufungaji Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, 12 yote amefunga kwa mguu wa kulia.

MTANZANIA MADINA IDDI ASHINDA MASHINDANO YA GOFU KENYA

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana ametoa pongezi kwa Mtanzania, Madina Iddi kwa kuibuka wa kwanza katika mashindano ya Gofu ya Muthaiga Ladies Open 2023 yaliyomalizika hivi karibuni nchini Kenya.  Mhe. Chana ametoa pongezi hizo Mei 21, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifunga  Mashindano ya Gofu ya Lugalo Ladies Open 2023, ambapo  ametoa Rai kwa Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali hususani mchezo wa Gofu kwa kuwa katika dunia ya sasa michezo inatoa fursa ya ajira. "Nalipongeza JWTZ na Klabu ya Gofu Lugalo kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi kutumia Klabu hii katika kuendeleza vipaji vyao na kukuza mchezo wa Gofu ambao unaendelea kukua siku hadi siku" amesema Mhe. Chana. Awali Mwenyekiti wa Lugalo Gofu Club Brigedia  Jenerali  Mstaafu, Michael Luwongo  amesema mashindano hayo yameshirikisha wanamichezo takriban 100 ambapo Wanawake ni zaidi ya 50.

DENVER NUGGETS WASHINDI WA NBA WESTERN CONFERENCE

Image
TIMU ya Denver Nuggets imeingia Fainali za Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya ushindi wa pointi 113-111 dhidi ya Los Angeles Lakers kwenye Fainali ya Western Conference Alfajiri ya leo. Pongezi kwa Nikola Jokic aliyefunga pointi 30, rebounds 14 na assists 13 na kuivusha Denver Nuggets kwa ushindi wa jumla ya Series 4-0. Mfungaji Bora wa muda wote wa NBA, LeBron James akiwa katika mechi ya mwisho msimu wake wa 20 kwenye histora yake ya NBA amejiwekea rekodi binafsi kwa kufunga pointi 31 kwenye first half ya Game 4. Mwamba huyo mwenye umri wa miaka 38, James kwa ujumla amefunga pointi 40, rebounds 10, assists tisa ingawa haikumsaidia Mfungaji huyo Bora wa muda wote wa NBA kuinusuru Lakers na kipigo cha nne mfululizo.

JUVENTUS YAPOKONYWA POINTI 10 SERIE A KWA UDANGANYIFU

Image
KLABU  ya   Juventus  imepokonywa   pointi   10  kufuatia   kusikilizwa   upya   kwa   kesi   yao   juu   ya tuhuma   za   udanganyofu   katika   malipo   ya uhamisho   wa   wachezaji . Awali ,  Juve   ilihukumiwa   kupokonywa   pointi   15  mwezi   Januar i ,  lakini   Korti   Kuu   zaidi   ya Michezo   nchini   humo   ikaagiza   shauri   hili lipitiwe   upya   mwezi   April i   na   huku   mpya imetolewa   jana   kabla   ya   kipigo  cha  4-1  kutoka kwa   Empoli . Adhabu   hiyo   inaiporomosha   Juve   hadi   nafasi   ya saba   katika   msimamo   wa   Serie A,  hivyo kupoteza   nafasi   ya   kucheza   michuano   ya   Ulaya msimu   ujao . Tayari   Napoli  imetwaa   ubingwa   wa   Serie A   na kabla   ya   hukumu   hiyo   ya   Jumatatu ,  w alikuwa tayari   wanaizidi   wanaizidi   pointi   17  Juve waliokuwa   nafasi   ya  pili .

WACHEZAJI SIMBA SC WAPEWA MAPUMZIKO TENA

Image
BENCHI la Ufundi la Simba SC limewapa mapumziko wachezaji wake hadi Jumatano kufuatia kusogezwa mbele kwa mechi mbili za mwisho za kumalizia msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. “Baada ya mchezo ujao wa Ligi Kuu kusogezwa hadi Juni 6, 2023, makocha wetu wametoa mapumziko kwa wachezaji na sasa watarudi kuendelea na mazoezi siku ya Jumatano Mei 24, 2023,” imesema taarifa ya Simba SC leo. Bodi ya Ligi imesogeza mbele mechi hizo ili kupisha michezo miwili ya Yanga ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili wiki hii Dar es Salaam na Juni 3 Jijini Algiers. Sasa mechi hizo za kumalizia msimu zitachezwa Juni 6 na Juni 9 na baada ya hapo itafuatia Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC) katĂ­ ya Azam FC na Yanga Jijini Tanga.

MAMILIONI YA MAMA, RAIS SAMIA YATUA YANGA

Image
MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akimkabidhi Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji kiasi cha Sh. Milioni 20, zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mabao mawili waliyofunga katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Marumo Gallants kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Jumatano iliyopita Jijini Rustenburg nchini Afrika Kusini.

SINGIDA BIG STARS 0-1 YANGA SC (KOMBE LA TFF)

Image
 

MAYELE AIPELEKA YANGA FAINALI ASFC

Image
MABINGWA watetezi, Yanga  wamekata tiketi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuwachapa wenyeji, Singida Big Stars 1-0 leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 82 akimalizia mpira uliookolewa na kipa Benedict Haule kufuatia shuti la winga mzawa, Dennis Nkane. Sasa Yanga ambao tayari wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo, itakutana na Azam FC katika Fainali ya Azam Sports Federation Cup baadaye mwezi huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Yanga sasa wanarejea Dar es Salaam kuanza kujiandaa na Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana Juni 3 Jijini Algiers nchini Algeria.

LIGI KUU YA TANZANIA BARA 2022-2023 KUHITIMISHWA JUNI 9

Image
MECHI za kufungia msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wa 2022-2023 zitachezwa Juni 9, kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB).

NOTTINGHAM WAIPA UBINGWA MAN CITY...WAIPIGA ARSENAL 1-0

Image
  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Arsenal jana kuchapwa 1-0 na Nottingham Forest Uwanja wa The City Ground, Nottingham, Nottinghamshire. Bao pekee la Nottingham Forest lilifungwa na mshambuliaji Mnigeria, Taiwo Micheal Awoniyi dakika ya 19 na sasa Manchester City ni mabingwa kwa sababu pointi zao 85 katika mechi 35 haziwezi tena kufikiwa na timu yoyote.  Nottingham Forest wanafikisha pointi 37 katika mchezo wa 37, ingawa wanabaki nafasi ya 16, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 81 za mechi 37 nafasi ya pili, ambako hakuna wa kuwapita kutoka chini.

WYDAD YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA

Image
MABINGWA watetezi, Wydad Athletic Club wametoka nyuma mara mbili kupata sare ya 2-2 na wenyeji, Mamelodi Sundowns katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, Afrika Kusini. Mabao ya Mamelodi Sundown yamefungwa na Themba Zwane dakika ya 50 na Mnamibia Peter Shalulile dakika ya 79, wakati ya Wydad yamefungwa na Ayoub El Amloud dakika ya 72 na Mothobi Mvala aliyejifunga dakika ya 83. Kwa matokeo hayo, Wydad inanufaika na mabao ya ugenini baada ya sare ya awali nyumbani ya bila kufungana Jijini Casablanca nchini Morocco. Watakutana na mabingwa wa kihistoria, Al Ahly ya Misri katika marudio ya Fainali ya msimu uliopita. Al Ahly imeitoa Esperance ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4-0, ikishinda 3-0 ugenini na 1-0 nyumbani.

MUZAMIL MZAWA PEKEE TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU

Image
KIUNGO wa Simba SC, Muzamil Yassin ndiye mchezaji pekee mzawa aliyeingia kwenye kipengele cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2022-2023. Muzamil anakwenda kuchuana na mchezaji mwenzake wa Simba, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza, kiungo Mbrazil wa Singida Big Stars, Bruno Gomes na nyota wawili wa Yanga, kipá Djigui Diarra kutoka Mali na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.