MMOJA AFARIKI, 30 WAJERUHIWA YANGA NA USM ALGER DAR


WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewajulia hali majeruhi 10 wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke waliojeruhiwa kutokana na tukio la kukanyagana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wakijiandaa kuingia kutazama mechi kati ya Yanga na USM Alger ya nchini Algeria katika mchezo wa Kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliocheza Mei 28, 2023.
Chana alipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Joseph Gasper Kimaro kwamba, walipokea majeruhi 30 ambapo wanaume walikua 18, Wanawake 10 na mtoto Mmoja ambapo mgonjwa mmoja alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.
Ameeleza kuwa mpaka sasa wamebakiwa na wagonjwa 10 na wote wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.
Chana katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwanahamisi Munkunda.
Taarifa ya awali ya tukio hilo ilitolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye alisema; “Hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea Majeruhi 30 ambapo 1 amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40”.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA