SIMBA SC YAFA KIUME CAIRO, YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI


TIMU ya Simba SC imetupwa nje ya michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali leo Uwanja wa Cairo International, Misri.
Kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute alianza kuifungia Simba dakika ya 68 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama kabla ya mshambuliaji Mmisri, Mahmoud Abdulmonem Abdelhamid Soliman ‘Kahraba’ kuisawazishia Al Ahly dakika ya 76 akimalizia pasi ya beki Mtunisia, Ali Maâloul.
Simba inayofundishwa na Kocha Mbrazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ inatolewa kwa Sheria ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Sasa Al Ahly inasubiri kukutana na mshindi wa jumla katí ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Petro de Luanda ya Angola zinazorudiana baadaye leo Jijini Pretoria.
Mechi ya kwanza Mamelodi Sundowns walishinda 2-0 mjin Luanda.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA