TAIFA STARS YACHAPWA 2-0 NA MOROCCO DAR, ZIYECH AKOSA PENALTI


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imechapwa mabao 2-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 uliofanyoka Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam leo.
Katika mchezo huo wa kuwania tiketi ya Fainali zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani, mabao ya Morocco yamefungwa na kiungo wa Galatasaray ya Uturuki, Hakim Ziyech dakika ya 28 na beki wa Azam FC, Lusajo Maaikenda aliyejifunga dakika ya 53.
Morocco ingeweza kuondoka na ushindi mtamu zaidi kama beki wake, Achraf Hakimi anayechezea PSG asingepiga juu mkwaju wa penalti dakika ya tatu.
Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wake, Novatus Dismas Miroshi anayechezea Shakhtar Donetsk ya Ukraine kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 65.
Wakati Taifa Stars ilianza kwa ushindi wa ugenini 1-0 dhidi ya Níger Jumamosi bao pekee la kiungo mshambuliaji Charles William M'Mombwa, Morocco imeanza kibarua leo kwa sababu waliopaswa kuwa wapinzani wao wa kwanza kwenye mbio hizi, Eritrea wametoa na sasa Kund E pamoja na Taifa Stas na Simba wa Atlasi – timu nyingine ni Kongo ‘The Red Devils’ na Zambia ‘Chipolopolo’.
Zambia walioanza na ushindi wa 4-2 Ijumaa dhidi ya Kongo Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola, leo wamechapwa 2-1 na Níger Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA